FALME ZITAKAZOWAATHIRI WATU WA MUNGU
(SEHEMU YA PILI)
(SOMA DANIELI 7:7-14,18,20-28)
Karibu tena rafiki tunapoendelea na unabii wa kitabu cha Daniel somo la nyuma linatupa ufunguo tunapoendelea na hii sehemu ya pili kumbuka Katika Sehemu hii ya Pili tuna kazi moja tu ya kufanya; kuthibitisha kwamba "Pembe Ndogo" inawakilisha Ufalme wa Papa au Upapa kama baadhi ya ndugu wamejaribu kuuliza hivi hii pembe ni kitu gani? wengine wakauliza alama au chapa ya mnyama ni IPI ninakutoa shaka Mpendwa haya yote kila mtu anatamani kuyaelewa vyema utayaelewa endelea kufuatilia masomo haya ,hata sura hii imegusia hayo maswali , pia sura ya nane imeweka wazi pia katika hilo .ilituweze kuitambua vyema hii pembe ndogo lazima tuangalie sifa zake , unajua watu iliwaweze kumkamata wachawi wana vigezo vyao vinavyothibitisha kuwa huyo kweli ni mchawi.
Mungu naye ameweka vigezo vyake ili kumtambulisha "Pembe Ndogo" na kuondoa mashaka yo yote waliyo nayo watu kuhusu suala hilo. Tutatumia mafungu ya Biblia huku na huku (Isa. 28:10) pamoja na Ushahidi wa Historia.
Kwa nini tusumbuke kuutambua ufalme huo?
Kwa sababu ufalme huo utasababisha wanadamu wote duniani watakaoambatana nao kuangamizwa pamoja nao (Ufu.19:11-21).
Kama nilivyosema huko nyuma, ufalme huu una majina mengi katika kitabu cha Danieli na kile cha Ufunuo.
Tutajaribu kujenga daraja la kuunganisha Danieli 7 na Ufunuo 13 kwa kuangalia vigezo vichache tu miongoni mwa vingi. Hukumu iliyotajwa katika Danieli 7 imeamua kumwondolea ufalme na kumwangamiza, lakini baada ya kupewa utawala wake wa Awamu ya Mwisho (Dan. 7:26; Ufu. 19:1-3; 18:4-8; 16:1,2,10,19-21; 17:1-11). Hebu na tuziangalie hizi Sifa za pembe ndogo iliyozuka kati ya zile kumi na kuziondoa tatu .
KIGEZO 1: PEMBE NDOGO ILIKUJA BAADA YA FALME 10 KUJITAWALA (Dan.7:8)
Falme 10 za Ulaya Magharibi zilizotajwa katika Sehemu ya Kwanza ya somo hili zilijitawala mwaka 476 B.K. mara tu baada ya Ufalme wa Warumi kuangushwa.
Baada ya kuanguka ufalme huo Askofu wa Rumi, ambaye baadaye aliitwa Askofu wa Maaskofu au Papa, alitawala katika mji wa Roma tu mpaka mwaka 538 B.K. alipoitawala Ulaya Magharibi. Historia inaunga mkono.
KIGEZO 2: PEMBE NDOGO ILIZING'OA PEMBE TATU KABLA YA KUTAWALA
Falme tatu zilizong'olewa kwa amri ya Papa (Dan. 7:8,20,24) ni hizi - Waheruli waling'olewa mwaka 493 B.K.;
Wavandali (Vandals) waling'olewa mwaka 534 B.K.;
Waostrogothi (Ostrogoths) waling'olewa mapema mwaka 538 B.K.
Kwanini haya mataifa yaling'olewa na huu ufalme.?
Mataifa hayo matatu yalikuwa yanampinga Papa.
Yale mengine 7 kufikia mwaka 508 B.K. yalikubali kuwa wakatoliki kwa kulazimishwa na mfalme wa Ufaransa, Clovis, mwana mpendwa wa Papa. Historia inathibitisha.
KIGEZO 3: PEMBE NDOGO ILIKUWA TOFAUTI NA PEMBE ZILE KUMI (Dan. 7:24).
Je utofauti wake ukoje ?
Pembe 10 ni falme za kisiasa za Ulaya Magharibi.
Pembe Ndogo ni Ufalme wa Papa wa Kidini-Kisiasa. Historia inaunga mkono.
Kanisa la Kikristo ulimwenguni halina utawala wa kisiasa (Yoh. 18:33-38). Kwa hiyo, Ufalme wa Papa umepata mamlaka yake kutoka kwingine, si kwa Mungu ,soma mafungu haya rafiki . (Ufu. 13:1,2; 12:9). Hii ndiyo maana wanaouunga mkono wataangamizwa pamoja nao.
Serikali zote za kisiasa za dunia zimepewa mamlaka yao na Mungu (Rum. 13:1-7; 1 Tim. 2:1-6). Kwa ajili hiyo zinawaadhibu wahalifu na kuwasifu raia wema. Ufalme wa Papa unawaua watu wema (watakatifu) na kuwaacha hai wahalifu soma rafiki hapa (Dan. 7:21)
KIGEZO 4: PEMBE NDOGO ILITAWALA KWA MIAKA 1260
Ninaomba rafiki hapa twende taratibu ilituelewane soma (Dan. 7:25). Katika biblia Wakati mmoja ni sawa na mwaka mmoja.
Kwa hiyo wakati 1 + 2 + 1/2 = Nyakati 3 1/2 = Miaka 3 1/2.
Mwaka 1 una miezi 12.
Kwa hiyo, miaka 3 1/2 = Miezi 3 1/2 x 12 = Miezi 42. Mwezi wa Biblia una siku 30 (Dan. 6:7; Mwa. 7:24). Kwa hiyo miezi 42 = siku 42 x 30 = siku 1260. Siku 1 ya unabii = mwaka 1 wa kawaida. Hivyo siku 1260 ni miaka ya kawaida 1260.
Angalia maajabu! Mnyama yule wa Ufunuo 13:1-10,18 alipewa kufanya kazi yake kwa miezi ile ile 42 (Ufu. 13:5). Ajabu zaidi ni kwamba Joka lile Kubwa Jekundu la Ufunuo 12 linawakilisha Rumi ya Kipagani iliyotaka kumwua Kristo kupitia kwa Herode (Ufu.12:2-5; Mt. 2:16) na tena linaiwakilisha Rumi ya Kipapa (Ufu. 12:6,14) ambapo tunaona mwanamke (kanisa la Mungu la kweli) akikimbilia nyikani kwa siku 1260 au miaka 1260. Kigezo hiki kinajenga daraja ya kuitambua Pembe Ndogo ya Danieli 7 kuwa ni Mnyama yule kama Chui wa Ufunuo 13. Tabia zinalandana sana.
Upapa ulitawala kihistoria kuanzia 538 hadi 1798 B.K., miaka 1260 kamili.
KIGEZO 5: PEMBE NDOGO ILIWAUA WATAKATIFU (Dan. 7:21,25).
Zaidi ya watatifu milioni 50 waliuawa katika kipindi cha utawala wa papa cha miaka 1260 kwa kosa la kufuata mafundisho ya Biblia. Aliwaita "wazushi" (heretics); Biblia inawaita "watakatifu". Ni kweli upapa ulikuwa umelewa kwa damu ya watakatifu (Ufu. 17:6).
Ni jambo la kushangaza mno kwa kanisa kuua kanisa! Linganisha na Ufu. 13:7. Ni ufalme ule ule mmoja.
KIGEZO 6: PEMBE NDOGO ILIAZIMU KUBADILI MAJIRA NA SHERIA (Dan. 7:25).
Sheria ni Amri Kumi za Mungu (Kut. 20:3-17). Upapa uliazimu kuifuta kabisa Amri ya Pili inayokataza ibada ya sanamu. Angalia Katekisimu za Kanisa Katoliki pamoja na Misale utashangaa. Amri ya Nne inayohusu Sabato akaibadili na kuweka Jumapili badala yake.
Kwa hiyo ibada ya Jumapili iliwekwa na Papa kinyume cha Amri ya Nne. Katika kitabu cha Ufunuo Jumapili inaitwa "chapa" au "alama" ya Mnyama, yaani, Alama ya Mfalme Papa (Ufu. 13:l6,17).
Katika gazeti la The Catholic Record, London, Ontario, la Septemba 1, 1923 maneno haya yamenukuliwa:
"Jumapili ni alama yetu ya mamlaka.... Kanisa li juu ya Biblia, na uhamishaji huo wa utunzaji wa Sabato [Jumamosi] ni ushahidi wa ukweli huo." Sasa zikawa zimebaki Amri 9, sio 10. Akaigawa Amri ya 10 katika amri mbili kufidia ya pili iliyofutwa kabisa.
KIGEZO 7: PEMBE NDOGO INANENA MANENO MAKUU YA MAKUFURU (Dan.7:8,20)
Hapa tutaangalia makufuru mawili tu.
Kufuru la kwanza ni madai ya kuwa yeye ni Mungu (Yoh. 10:30-33).
Kwa vipi? Nanukuu: "Papa ana cheo kikubwa mno, tena ametukuzwa mno kiasi kwamba yeye si mwanadamu tu, bali kama ilivyo ni Mungu, tena ndiye aliye Badala ya Mungu."
----- Lucius Ferraris, Prompta Bibliotheca Canonica, Gombo la VI, uk. 438,442, chini ya makala "Papa". Cheo cha Mungu alichojinyakulia ni "Baba Mtakatifu" (Yoh. 17:11).
Kufuru la pili ni kudai kuwa anao uwezo wa kusamehe dhambi
jukumu ambalo ni la Mungu peke yake (Luka 5:20,21).
Mungu peke yake ndiye anayeabudiwa (Mt. 4:10); lakini papa anataka aabudiwe (2 The. 2:3,4; Ufu. 13:4,7,8,12). Linganisha na Ufu. 13:1,5,6.
Ni mamlaka moja ile ile.
Mungu hataki watu wake wawe gizani kuhusu ufalme huu, japo kwa sasa ulimwengu unauinua juu sana. Hatimaye utakapotawala kama alivyoruhusu Mungu itakuwa kwa maangamizi ya ulimwengu mzima na dunia itafikia mwisho wake (Ufu. 17:811; 6:14-17; 19:11-21). Usiwe miongoni mwa wale wanaofanya mambo kwa kupelekwa bila kujua ashukuriwe Mungu maana amekuonesha baadhi ya siri juu ya hii pembe ndogo .kumbuka mwisho wa haya yote kutakuwa na makundi mawili ,wale wanaokubali kuteswa kimwili kwaajili ya ukweli ,na wale watakaopoteza hata nafsi zao kwa mauti ya milele,tutaendelea na sura ya saba lakini kumbuka kwamba wale watakaosimama katika kweli yote wakipingana kwa imani dhidi ya hii pembe watakwenda mbinguni kutawala pamoja na Yesu kwa miaka 1000 (l The. 4:16,17(18); Ufu. 20:4). Dunia hii itakuwa imeharibika vibaya kipindi chote cha miaka 1000 (Yer. 4:23-27). Baada ya kwisha miaka 1000 watakatifu watarudi hapa pamoja na Mji Yerusalemu Mpya (Ufu. 21:10).
Ndipo waovu watakapofufuliwa na kujaribu kuuteka Mji Yerusalemu Mpya au Kambi ya Watakatifu. Moto utawala (Ufu. 20:7-10,15). Hiyo ndiyo Jehanum au Ziwa la Moto au Mauti ya Pili (Ufu. 20:14). Jehanum haiwaki sasa. Itawaka baada ya miaka ile 1000 kwisha. Watakaoingia humo watateketezwa na kuwa majivu pamoja na Shetani na malaika zake( Mal. 4:1-3; Eze. 28:14-19).
Hawatafufuliwa tena milele! Ndipo watakatifu watakapoirithi nchi mpya (Ufu. 21:1; Mt. 5:5; 2 Pet. 3:10-13; Zab. 37 yote).
NInaomba tuwe miongoni mwa watakatifu wanaosimama katika maandiko nasio mapokeo hawa wanajurikana ,wao biblia na biblia pekee ndio msingi wao na ndio wanaoendelea kukuletea habari njema zisizofundishwa mahali popote pengine ,ninakuarika Mpendwa endelea kufuatilia masomo haya ,Fanya tafakari moyo ni mwako ,omba Mungu akufungue zaidi ,nnaamini katika Kristo atakubariki .
Karibu kwa somo linalofuata sura ya nane.

ConversionConversion EmoticonEmoticon