FALME ZITAKAZOWAATIRI WATU WA MUNGU .

FALME ZITAKAZOWAATHIRI WATU WA MUNGU

(SEHEMU   YA   KWANZA)

(SOMA  DANIELI  7  YOTE) Mpendwa na rafiki katika Kristo ninakukaribisha tena siku ya leo tunapoendelea na kitabu cha Daniel leo tunaanza hasa siri nyingi na kubwa ambazo zipo katika biblia ,katika sura hii ya saba ni falme zilezile tulizoziona katika sura ile ya pili ila hapa kuna zaidi ya Maelezo yale ya sura ya pili kwa kuuelewa zaidi tutaigawa  sehemu  mbili  ili  iwe  rahisi  kufuatilia.

Sehemu ya Kwanza itatoa  picha  ya  falme  zote  kuanzia  Babeli  hadi  atakapokuja  Bwana Yesu  kuusimamisha  ufalme  wake  wa  milele.    
Sehemu  ya  Pili  itahusika  na  Ufalme  wa Pembe Ndogo ambao utawaathiri sana watu wa Mungu katika  siku  za  kufungia  historia ya ulimwengu  huu.   Watu  wa  Mungu ni  Israeli  ya  Kimwili  (Wayahudi)  na  Israeli  ya  Kiroho (Wakristo wa Mataifa yote).    Soma  Warumi  2:28,29 na Wagalatia 3:26-29, na  kurudia somo la Danieli  9  juu  ya  Taifa Takatifu  la  Mungu la  siku hizi.
 Katika  Danieli 2 tuliziangalia falme hizo kwa Mtazamo wa Kisiasa.   Tuliangalia  tu utukufu wa falme  hizo uliopungua  kulingana na madini  -----  dhahabu, fedha,  shaba,  chuma,  na  udongo.  
 Babeli ulikuwa  na  utukufu  kuliko zote (Isa. 13:19).
 Katika Danieli  7  tunaziangalia  falme  hizo  kwa  mtazamo  wa  KidiniKisiasa. Tunaona  jinsi falme  hizo  zilivyowaathiri watu  wa  Mungu  (Israeli ya  Kimwili  na  Israeli ya Kiroho).
JE unadhani Mungu haoni watu wake wanapoteswa ?
 Mungu anatishia kuchukua hatua ya kuziangamiza falme zote zinazotesa na kuwaua watu wake (Yer. 25:15-38;  46:28);  watu wa Mungu ni sawa na mboni ya  jicho lake  (Zek.  2:8).   Kuwapiga  vita  watu  wa  Mungu  ni  sawa  na  kupigana  na  Mungu mwenyewe.   Kilele  cha  Pambano  hili  ni  Vita  ya  Har-Magedoni  ambayo  ni  vita  kati  ya Mungu na falme za dunia zinazotaka kuwaua  watu wake,  na  kwa  kufanya hivyo  zinapigana na  Mungu  mwenyewe (Ufu. 16:13-16).   Tutaona jinsi mataifa  hayo moja  baada ya jingine falme zao  zilivyokomeshwa  kabisa.   Ufalme  wa Warumi  wa  Kipagani  na Ufalme  wa Rumi ya Kipapa utapatilizwa  katika nyakati  za Agano Jipya  kwa njia ya zile  Baragumu Saba za Ufunuo 8 hadi 11.   Utaelewa vizuri tukianza kitabu cha ufunuo.
Ni jambo la kusikitisha  mno  kwamba  falme zote za dunia  tamati yake ni kuangamizwa vibaya kwa sababu  tu ya kumsaidia huyo  "Pembe Ndogo" aitwaye kwa jina lingine "Mnyama" (Ufu. 19:11-21). Utaelewa vyema tukianza kitabu cha ufunuo.
  Ni jukumu letu kuwaombea sana Wafalme,  MaRais, mawaziri  na  viongozi  wote  wakuu  wa ngazi  zote katika  serikali  zote  duniani  ili  wasije wakapatwa na mkasa huo aliouandaa Ibilisi (1 Tim. 2:1-6). Maneno  ya  kawaida  tunayotumia  mitaani  yana  maana  tofauti  katika  taaluma mbalimbali.   Kwa  mfano  "kijiko"  ni  chombo  tunachotumia  kulia  chakula;    lakini  kwa Mhandisi wa Majengo na Barabara "kijiko" ni aina fulani ya  katapila  linalochota  udongo na kuuweka wanakotaka.

 Kwa mtu mwenye akili ni muhimu kuuliza,  "Una maana gani kusema  hivyo?"   Ufafanuzi utakapotolewa harara  yake  itapoa.   Hivi  sasa  watu  wanaposikia neno hili "Mnyama" hasira zao zinapanda juu  kiasi cha kumpa mikong'oto anayelitamka, hata  kumpeleka  mahakamani.    Lakini  neno  hilo  limetumika  katika  taaluma  ya  unabii, maana  ya  "Mnyama"  ni "Mfalme" au "Ufalme" (Dan.7:17).   Nani  atampa  mikong'oto  mtu anayesema  "Mfalme"?   Atakuwa  na  upungufu kiakili. Ya nini  kufoka,  ndugu  yangu?   Uliza kwanza, utapata maana yake.  Kwa hiyo, huyo  Pembe  Ndogo  ni  Mfalme  au  ni  Ufalme.  Tutatumia Sehemu ya Pili kumfafanua ili kila mtu amjue.    Kwa  maana  asipojulikana  na watu  wote  duniani,  Yesu  Kristo  haji;   tutaendelea  kusota  duniani  na  kuteseka  kwa magonjwa  sugu,  umaskini,  dhuluma  kwa  muda  usiojulikana  (2  The.  2:1-4).    Paulo amerahisisha sana kwa wale wasioujua unabii kumtambua mfalme  huyo katika  fungu  la 4.
Hebu  sasa  na  tuziangalie  falme  hizo  kwa  jumla.    Wanyama  wote  waliotajwa  ni wakatili.  Hii inamaanisha kwamba falme hizo zilifanya ukatili mkubwa.  Tutapitia kwa kifupi tu:

1. SIMBA  -----  UFALME WA BABELI

(*606-538 au 605-539 K.K.)
Ufalme wa  Babeli  unawakilishwa  na  Simba  (Dan.  7:4;    Yer.  4:5-7;    Hab.  1:6-8). Katika  Danieli  2
umewakilishwa  kwa  Kichwa  cha  Dhahabu  (Dan.  2:37,38).    
Kuhusu ukatili wake soma
2 Nya.  36:17-20;  Yer. 21:7.   "Mabawa mawili"  aliyokuwa nayo simba ni kasi au  wepesi  wa kushinda  vitani  (Hab.  1:6-10).   *Vitabu  vya  historia  huonyesha  miaka tofauti.

2. DUBU  -----  UFALME WA WAMEDI NA WAAJEMI
(*538 au 539-331 K.K.)
Ufalme  wa Wamedi na  Waajemi unawakilishwa na  Dubu,  mnyama  mkali  sana  (Dan. 7:5).  Katika  Danieli  2 umewakilishwa  na  Kifua  na  Mikono  ya Fedha (Dan. 2:39a;  5:2531).   "Mbavu  3"  ni  majimbo  matatu  yaliyotekwa  kikatili  sana  na  ufalme  huu,  nayo  ni Babeli, Misri, na Lydia  (sio Libya).   Kuhusu ukatili wake  soma Isa. 13:17-22;  Yer. 51:2844.

3. CHUI  -----  UFALME WA WAYUNANI

(331-168 K.K.)
Ufalme wa Wayunani unawakilishwa na Chui, mnyama mwenye machachari  sana (Dan. 7:6). Katika Danieli 2 umewakilishwa  na  Tumbo  na  Viuno  vya  Shaba (Dan. 2:39b;  8:20,21). "Mabawa  manne"  humaanisha  kasi  zaidi  katika  kushinda  vitani.    "Vichwa  vinne" huwakilisha watawala au wafalme   (Ufu. 17:9,10)  wanne waliotawala baada  ya  kufa  Iskanda Mkuu (Alexander the  Great).   Hao  ni majenerali wake  -  Cassander, Lysimachus, Seleucus, na  Ptolemy.   Katika  Danieli  8  Iskanda  Mkuu  ni  "pembe  mashuhuri  kati  ya  macho  ya beberu" (Dan. 8:5,21), majenerali hao  wanne  ni  "pembe  nne"  za  beberu  (Dan.  8:8,22). Ukatili wa ufalme huu soma Dan. 8:6,7.

4. MNYAMA WA KUTISHA   -----  UFALME WA WARUMI
 (168 K.K. - 476 B.K.)

Ufalme wa Warumi unawakilishwa na mnyama wa kutisha asiye  na  jina,  mwenye pembe  10  (Dan.  7:7).    Ulitawala  makoloni  10  ya  Ulaya  Magharibi.    Katika  Danieli  2 umewakilishwa na  Miguu  ya  Chuma  (Dan. 2:40).  Ukatili  wake soma Dan.  7:7,23;  2:40. Ni  ufalme  unaovunja-vunja.  Hawakutajwa  kwa  jina  ila  historia  inakiri  kuwa  utawala uliouangusha Uyunani  ni  Rumi mwaka  168  K.K.  Yesu  alipozaliwa ulikuwa  bado  unatawala(Luka 2:1-7;  Yoh. 11:48).

5. PEMBE KUMI  -----  FALME 10 ZA ULAYA MAGHARIBI

(476 B.K. -  KUJA YESU)
Falme  hizo  zinawakilishwa  na  Pembe  10  (Dan.  7:8).   "Pembe"  ni  "Wafalme"  au "Falme"  (Dan.  7:24).    Falme  10  zilijikomboa  toka  ukoloni  wa  Kirumi  ulipoangushwa mwaka  476  B.K.  na  mataifa  ya  kipagani  ya  Ulaya  Kaskazini.  

Falme  10  ni  

Uingereza, Ufaransa,  Ujerumani,  Uswisi  (Switzerland),  Ureno,  Hispania,  Italia,  Heruli,  Wavandali (Vandals), na Waostrogothi (Ostrogoths).  
Katika Danieli 2 zimewakilishwa na  Vidole 10 vya Nyayo (Dan.  2:41,42).    Kuhusu  ukatili  wao  soma  historia.   Zilimsaidia, tena  zitamsaidia papa kuua watakatifu (Ufu.17:12-14).

 6. PEMBE NDOGO  -----  UFALME WA PAPA AU UPAPA

(538-1798 B.K.)
Ufalme wa Papa hapa unawakilishwa na Pembe Ndogo (Dan. 7:8,20,24).    Ufalme huu una majina mengi katika unabii  -----  Chukizo  la  Uharibifu,  Mnyama,  na  kadhalikaUmewakilishwa na  Nyayo za Miguu  (2:33,42).   Ukatili  wake  usio  na  kifani  ulidhihirika katika  Zama  za  Giza  (Dark  Ages)  ulipowaua  zaidi  ya  milioni  50  ya  watu  wa  Mungu uliowaita  "Wazushi"  (Heretics).   Soma  Dan.  7:21,25.  

Tunajuaje  kama  huo  ni  Upapa?

Soma Sehemu ya Pili ya Danieli 7 itakayofuata baada ya hii ..

7. MMOJA  ALIYE  MFANO  WA  MWANADAMU  --  UFALME  WA  KRISTO (AJAPO)

Ufalme  wa  milele  wa  Kristo  umewakilishwa na Mmoja aliye  Mfano  wa  Mwanadamu (Dan. 7:13,14; Mt. 24:29-31).   Katika  Danieli 2 uliwakilishwa na  Jiwe  (Dan.  2:34,35,44,45).  Ufalme huu hauna ukatili; raia zake watakuwa  na  amani  milele  (Ufu.  7:13-17;    21:l-7). Lakini  kabla  ya  ufalme  huo  kuja,  Hukumu  inaendelea  mbinguni  tangu  1844  kuamua hatima  ya falme  hizo  zinazotesa watu  wa  Mungu  pamoja  na  adhabu  ya  waovu  wote;  ndipo atakuja mfalme wa amani je, ikotayari kumlaki ajapo usiwe na shaka Mpendwa wokovu upo kwaajili yako ,uendelee kufuatilia haya masomo utajifunza zaidi hata YESU atakapokuja hautaogopa bali utashangilia (Ufu.22:11,12).

Mpendwa nnaamini umeona baadhi tu ya mambo ambayo yamefichwa watu wengi hawayafundishi maana yanafunua ukweli ulivyo hasa ! Jipe moyo utaelewa usiwe na shaka ,Mungu atakufunulia zaidi ya hayo wewe umebarikiwa sana kuyafahamu haya ubarikiwe sana ,Karibu tuanoendelea na sehemu ya pili ukiwa na swali usisite kuuliza weka swali lako kwenye comments hapo chini ,
Previous
Next Post »