TAIFA TAKATIFU LA ISRAELI LAKATALIWA
(SOMA DANIELI 9 YOTE)
Huu ni muendelezo wa Daniel sura ile ya nane ambapo Daniel hakupata vizuri kuielewa tafsiri yake hapa tunaendelea na hiyo tafsiri katika sura ya tisa.
Kwahiyo Gabrieli alikuja tena kwa Danieli baada ya kupita muda fulani tangu siku ile aliyozimia ili kumpa maelezo zaidi ya maono yake ya Danieli 8. Unakumbuka Danieli alizimia (Dan. 8:27).
Kwa hiyo Gabrieli alishindwa kuendelea na maelezo yake; sasa akaja tena kummalizia maelezo ya maono yale (Dan. 9:20). "Muda wa majuma sabini umeamriwa [umekatwa, umetengwa kutoka katika kipindi kile cha miaka 2300] juu ya watu wako [Wayahudi], na juu ya mji wako mtakatifu [Yerusalemu].... Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake Masihi aliye Mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, Masihi atakatiliwa mbali.... Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu..." (Dan. 9:24-27). Kama ilivyo, juma moja lina siku saba, na siku moja ya unabii ni mwaka mmoja wa kawaida.
Kwa hiyo, majuma 70 ni siku 70 x 7 = siku 490 au miaka 490. Miaka hiyo inakatwa katika ile 2300 ya Danieli 8:14 na inaanza kuhesabiwa mwaka ule ule wa 457 K.K. ilipotolewa amri iliyofanikiwa ya kuujenga upya Yerusalemu.
Miaka hiyo 490 kuanzia 457 K.K. inaishia mwaka 34 B.K. Kipindi hicho walipewa Taifa Takatifu la Israeli ya kale ili kutekeleza mambo 6 yaliyotajwa. Walitakiwa kumpokea Masihi kama Mwokozi wao na kupewa haki yake. Lakini alipokuja kwao hawakumpokea kama Taifa (Yohana 1:11). Majuma 7 ni miaka 7 x 7 = miaka 49 kuanzia 457 K.K. hadi 408 K.K. Majuma 62 ni miaka 62 x 7 = miaka 434 kuanzia 408 K.K. hadi 26 1/2 au 27 B.K. Mwaka wa 27 ndio Yesu akajulikana kama Masihi [Mpakwa Mafuta] alipobatizwa na kushukiwa na Roho Mtakatifu (Mt. 3:13-17; Mdo. 10:38).
Ni kweli wakati ulikuwa "umetimia" kulingana na unabii wa Danieli 9 uliomhusu Masihi (Mt. 4:17). Majuma 7 + majuma 62 = majuma 69 au miaka 49 + 434 = miaka 483 tangu 457 K.K. ambayo iliishia 27 B.K. Kwa hiyo likawa limebaki juma 1 tu au siku 7 au miaka 7 tu kumaliza kipindi kile cha miaka 490 waliyopewa Taifa la Israeli kumpokea Yesu Miaka 490 - 483 = miaka 7 ambayo ingeishia 34 B.K. (27 + 7 = 34). Katikati ya juma la mwisho, yaani, nusu ya miaka 7 ni miaka 3 1/2 "Masihi atakatiliwa mbali" atauawa kikatili. Kwa hiyo 27 + 3 1/2 = 30 1/2 = 31 B.K. Kristo (Masihi) alisulibiwa. Unabii huu ulitimia barabara. Ingawa Taifa la Israeli lilimkataa Masihi katakata kuwa sio Mfalme wao (Yoh. 19:15), walikuwa wamebakiwa na kipindi cha miaka 3 1/2 hadi 34 B.K. cha kuhubiriwa Injili. Siku moja ilipokaribia Pasaka yake ya mwisho kabla hajaingia mjini aliulilia sana mji na kuusikitikia kwa kile kitakachoupata (Mt. 19: 41-44; Mt. 23:37-39). Alitabiri juu ya kuangamizwa kwa mji huo na majeshi ya Warumi mwaka wa 70 B.K. (Dan. 9:26b). Walikuwa wanajivunia hekalu, lakini yeye akawaambia wazi, "Angalieni nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa," yaani, utukufu wake umeondoka mle kuanzia siku ile.
Hotuba yake ndefu ya Mathayo 24 na 25 ilihusu matukio ya siku za mwisho. "Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe" (Mt. 26:1,2). Huo ulikuwa mwaka wa 31 B.K. Kipindi kifupi kabla ya Pasaka hiyo alikuwa amewaambia waziwazi kuwa "Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa Taifa lingine lenye kuzaa matunda yake" (Mt. 21:43). Ni taifa gani hilo? Kwa nini alisema maneno hayo kwao? (Mt. 21:33-46)Taifa lingine Takatifu la Israeli ni lipi? Lilipewa lini Ufalme wa Mungu? Bila shaka lilipewa ilipokwisha miaka ile 490 au majuma 70 waliyopewa Taifa la Israeli la zamani. Walikuwa bado wamebakiwa na miaka mitatu na nusu ya kuhubiriwa injili (30 1/2 + 3 1/2 = 34). Muasisi wa Taifa Jipya la Israeli ni Kristo mwenyewe. Aliwaagiza wanafunzi wake kuhubiri injili kwanza kwa "kondoo waliopotea wa Israeli" na kuwakataza wasiwaendee Mataifa (Mt. 10:6). Hatimaye aliwaambia, "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi [dunia]" (Mdo. 1:8). Mwaka 34 B.K. Stefano alipigwa mawe, na mwaka uo huo injili ikaenda kwa Mataifa. Mwaka uo huo Paulo akawatangazia Wayahudi waliomkataa Masihi, akasema, "Ilikuwa lazima Neno la Mungu linenwe kwenu kwanza [umuhimu wa kwanza mpewe ninyi]; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa" (Mdo. 13:46).
Taifa la Israeli likawa limekataliwa. Tangu 34 B.K. si taifa takatifu tena; wala halijatengewa kipindi kingine maalum cha kuhubiriwa injili kama upendeleo kwao baada ya kanisa kunyakuliwa (1 The.4:16,17[18]). Hapatakuwa na mwanadamu hai duniani kanisa litakaponyakuliwa (Yer. 4:23-26). Waliuchezea muda wao waliotengewa na Mungu. Watahubiriwa injili pamoja na mataifa yote katika kipindi kimoja tu kuanzia 34 B.K. mpaka Kuhani Mkuu, Yesu Kristo, atakapofunga kazi yake ya Maombezi katika Hekalu la mbinguni (Ufu. 14:6-12; 15:8; 22:11). Kitakachofuata ni mapigo 7 ya mwisho (Ufu. 16 yote). Masharti yale yale aliyolipa Taifa Takatifu la Israeli la zamani ndiyo yale yale aliyolipa Taifa Takatifu la Israeli ya Kiroho au Wakristo (Kut. 19:5,6; 1 Petro 2:9,10; Ebr. 8:10). Utii kwa Amri Kumi ndio msingi wa Agano la Kale na Agano Jipya. Hii ndiyo maana "watakatifu" wa siku za mwisho kama wale wa zamani watakuwa wanazishika Amri Kumi za Mungu pamoja na Imani ya Yesu (Ufu. 14:12; 1 Yoh. 2:3-6). Imani ya Yesu inahusu kumpokea kama Mwokozi na kufuata mafundisho yake yote (Mt. 28:19,20; Mk. 16:15,16; Yoh. 3:16; 14:21-26). Wakristo wa mataifa mbalimbali wanaitwa "Wayahudi" au "Waisraeli" wa Kiroho (Rum. 2:28,29; 9:6-8; Gal. 3:26-29). Kifo cha Yesu msalabani kilifutilia mbali tofauti iliyokuwapo kati ya Wayahudi na Mataifa; wote sasa wako sawa na wana haki sawa kwa njia ya kumwamini Kristo (Efe. 2:11-22). Tungepiga kelele na kusema, "Bwana asifiwe!!!". Hakuna tofauti tena. Chini ya Msalaba ule wa Kalvari wanadamu wote ni sawa. Hakuna haja ya kuwatengea kipindi maalum cha kuwahubiri injili Wayahudi. Wanapaswa kuhubiriwa injili sasa; siku ya wokovu kwa kila mwanadamu ni sasa, sio baada ya kanisa kunyakuliwa (2 Kor. 6:2). Kulinyakua kanisa kutaambatana na kuangamizwa kwa yule Chukizo la Uharibifu na wote wanaomwunga mkono (Dan. 9:27; Ufu. 19:11-21).hili ni hakika kwamba chukizo la uharibifu litaangamizwa na wale wote watakaounga mkono madanganyo yake ,kama haya yote umepata kuyafahamu kwa nini usijinasue katika huu uangamivu ,endelea kutafakari huu unabii ukijitoa kwa YESU pekee ndiye atakupa uzima tele katika maisha yako ,Karibu kwa sura inayofuata ,kama Ukipata swali usisite kuuliza ,Bwana akubariki.

ConversionConversion EmoticonEmoticon