VITA VIKUBWA VINAENDELEA NYUMA YA PAZIA
(SOMA DANIELI 10 YOTE)
Karibu tena Mpendwa katika muendelezo wa neno la Mungu tunapoendelea na sura ya kumi kwa wale wageni usijisikie umekosa masomo hapana yote yapo katika hii blog.yafungue utayapata yote ,kumbuka kuwa katika dunia hii kuna vita vikali vinavyoendelea baina ya nuru na Giza yaani Kristo na shetani ,sisi ni kama chambo katika hii vita ,kwa namna flani uchaguzi wetu katika maisha ndio unaotuweka katika upande wa Kristo au wa shetani ,usisite kufanya uchaguzi mzuri wa kumfuata Kristo unapoendelea kujifunza neno lake, Karibu na Bwana akubariki.
Rafiki kumbuka kuwa ni jambo la kutisha mno kujulishwa kwamba vita vikubwa vinaendelea nyuma ya pazia; havionekani kwa macho yetu ya kibinadamu, ingawa matokeo yake tunayaona. Danieli alifunuliwa, yaani, alionyeshwa vita vikubwa hivyo visiyoonekana; akaelewa kile ambacho alikuwa hajapata kukielewa siku za nyuma (Dan. 10:1). Yohana pia akiwa Patmo alionyeshwa juu ya vita hivyo vikubwa kuanzia vilipoanza mbinguni na kuhamia hapa duniani hadi vitakapomalizika katika vita ile ya Har-Magedoni (Ufu. 12:7-17; 16:13-16; 17:12-14; 19:11-21).
Kumbe kuna nguvu kuu mbili zinapambana! ----- Mikaeli (Kristo) na malaika zake, na Joka (Shetani) na malaika zake. Ni Pambano Kuu kweli kweli! Wahenga walisema, "Fahari wawili wakigombana, nyasi zinateketea." Ndivyo ilivyo. Wanadamu ndio wanaoathirika sana katika Pambano hilo. Paulo anasema kwamba sisi tumekuwa "tamasha kwa dunia [malimwengu yote]; kwa malaika na kwa wanadamu (1 Kor. 4:9). Tutakimbilia wapi, maskini! Ajabu ni kwamba Pambano hilo linapiganwa ndani ya mioyo yetu, japo matokeo yake tunayaona nje. Tutawezaje kujihami? Paulo anasema tuvae silaha zote za Mungu ili tupambane na nguvu za giza, si kwa kutumia mabavu bali kwa kutumia Upanga wa Roho, yaani, Neno la Mungu, na Imani, na Maombi ya dhati (Efe. 6:10-20). Ayubu hakujua kilichokuwa nyuma ya mikasa iliyompata kwa mfululizo; lakini hatimaye alijua. Hatujui kwa nini mambo yanatuendea vibaya ingawa sisi tunaomba sana. Kumbe! nyuma ya mambo yote yanayotutatiza kuna vita vikubwa vinaendelea kati ya nguvu za wema na nguvu za uovu. Mungu angetufumbua macho yetu wengi wetu tungezimia kuona jinsi Shetani na malaika zake wanavyowafanya wanadamu au tungekata tamaa kabisa usishange hata katika kujifunza huu unabii jinsi changamoto ulivyoziona lakini jipe moyo Mungu atakufunulia zaidi. Unabii wote wa Danieli 2, 7, 8, 9, 11, 12; kitabu cha Ufunuo chote; Mathayo 24 unalihusu pambano hilo au vita hivyo vikubwa. Mungu ashukuriwe ya kwamba ushindi ni wa hakika kwa watu wa Mungu hata kama watakatwa vichwa au kufanyiwa jeuri yo yote (Ufu. 15:2; 20:4; 12:11; Ebr. 11:35-38; Rum.8:35-39).
Je, Shetani anafurahi watu wa Mungu wanapofanikiwa kufanya kazi ya Mungu? Hasha. Anaweka vipingamizi vingi ili kuzuia kazi ya Mungu isifanyike kabisa. Kazi ya Mungu inamnyang'anya raia zake aliodhani ni mateka wake; yeye hataki kuwachilia kamwe. Kinyume na shetani ambae anataka wote wapotee.
"Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao" (Isa. 14:17b). Hata wale waliomponyoka kwenda mkononi mwa Yesu anajaribu kuwapokonya tena (Yoh. 10:2730). Kwa hiyo, ni vita vikubwa vinavyoendelea nyuma ya pazia mpaka hapo vitakapozimwa na Mungu mwenyewe katika siku ile ya mwisho. Anaweza kutufunulia au anaweza asitufunulie. Kwetu sasa ni vizuri kuelewa tu kuwa tuko kwenye uwanja wa mapambano, na kwamba "hapa sipo mahali pa raha" yetu; uchafu umejaa na maangamizo mazito sana" (Mik. 2:10).
Tunamkuta Danieli amefunga kwa siku 21 akiomba ili Mungu aifanikishe kazi ya ujenzi wa Yerusalemu kama Koreshi alivyowatuma Wayahudi kuifanya kazi hiyo (Ezra 1:25). Kazi ile haikwenda vizuri; kulikuwa na vurugu nyingi kutoka kwa Wasamaria ambao hawakutaka hekalu lile lijengwe (Ezra 4). Mashtaka yakaenda kwa Koreshi ili atoe amri ya kusimamisha kazi ile. Kumbe wakati ule ule alipokuwa anaomba Danieli, mfalme Koreshi alikuwa anashawishiwa mawazoni mwake kuisimamisha kazi ile. Kumbe vita vikubwa vilikuwa vinaendelea kati ya Mikaeli (Kristo) na Shetani juu ya suala hilo.
Kristo akimshawishi Koreshi kuunga mkono kazi ile, na Shetani akimshawishi Koreshi kuikataza kabisa kazi ile aliyokuwa ametoa amri. Mapambano ya siku 21 yakaulainisha kidogo moyo wa Koreshi.Ndipo Mikaeli (Kristo) akaja kwa Danieli (Dan. 10:2-9; Ufu. 1:10-15).
Danieli alipotelewa na nguvu kabisa mbele za Kristo, akaanguka chini uso ukielekea chini na usingizi mzito ukamshika. Ndipo Gabrieli akamwinua na kumweka katika hali ya kusujudu na kumjulisha sababu ya maombi yake kuchelewa kujibiwa (Dan. 10:10). Kumbe sala ya Danieli ilikuwa imesikiwa siku ile ile aliyoanza kuomba (Dan. 10:12).
Kwa nini jibu lilicheleweshwa basi?
"Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli [Kristo], mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na Wafalme wa Uajemi [Kristo aliendelea kuwagusa mioyo wafalme wa Uajemi waliomfuata Koreshi]" (Dan. 10:13). Gabrieli alijaribu kumshawishi Koreshi kwa siku 21 bila mafanikio, ndipo akaja Kristo mwenyewe na kuugusa moyo wa Koreshi ili kazi ya ujenzi wa Yerusalemu isikwamishwe. Hata sasa malaika wa Mungu wanakuwamo katika Mabunge ya nchi mbalimbali yanayotunga sheria ili kuhakikisha sheria hizo hazitaiathiri kazi ya Mungu ulimwenguni.
Malaika waovu wanajaribu kuwashawishi Wabunge kutunga sheria zitakazoiathiri kazi ya Mungu; lakini malaika wa nuru wanapinga. Ni vita vikubwa hivyo nyuma ya pazia! Ipo haja kubwa ya kuiombea kazi ya Mungu duniani hasa, kwa wakati kama huu. Kwa nini Kristo alikuja kwa Danieli wakati kama ule? Kulikuwa na ujumbe kwa ajili ya siku hizi za mwisho. Gabrieli akampasha habari Danieli, "Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako [Israeli ya Kiroho] katika siku za mwisho; maana maono haya ni ya siku nyingi bado" (Dan. 10:14). Kutokana na maombi ya bidii ya Danieli alionyeshwa mambo yatakayowapata watu wa Mungu siku za mwisho. Alipewa nuru ya kuyaelewa maneno ya Mungu ya kweli. Gabrieli alikuwa tayari kumfunulia zaidi juu ya Maandiko, akasema, "Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli" (Dan. 10:21). Neno la Mungu ni kweli; linatutakasa tukifanya lisemavyo (Yoh. 17:17; 7:17; 1 Petro 1:22-25; Yak. 2:22). Shetani siku hizi anawashawishi Wakristo wasisome Neno la Mungu ati kwa sababu wanaongozwa na Roho.
Lakini kuna Roho Mtakatifu na "roho ya upotevu", nguvu zote mbili zinawaongoza watu (1 Yoh. 4:1,6).
Roho wa kweli kazi yake ni kutufundisha kweli, yaani, Neno la Mungu mpaka tulielewe vizuri kabisa (Yoh. 16:13-15; 14:21-26).
Roho ya upotevu inatukataza kusoma wala kusikia neno la Mungu. Yohana ametupa ruhusa kumpima Roho aliye ndani yetu, kujua ni wa aina gani, yaani, kama ni Roho wa Mungu kweli au ni roho ya upotevu.
Mtu anayesema "Mimi naongozwa na Roho," halafu anasema, "Sina haja ya kusoma, wala kulisikia neno la Mungu," huyo haongozwi na Roho Mtakatifu, bali ile roho ya upotevu au "roho zidanganyazo," yaani, "roho za mashetani" au "mapepo" (1 Tim. 4:1; Ufu. 16:13,14).
Neno la Mungu linatuimarisha sana, hata pepo zivume namna gani hazitatuangusha (Mt. 7:24-27). Jikite juu ya Mwamba, yaani, Neno la Mungu au Kristo (Ufu. 19:13; Yoh.1:1-3). Neno na Kristo ni kitu kimoja tu. Huwezi kumpokea Kristo; na kulikataa Neno lake. Usirushwe-rushwe na kila upepo wa mafundisho; omba upewe mafungu ya Biblia kwa kila fundisho, utakuwa salama (Efe. 4:11-15). Jitahidi kusoma Biblia; itakuhekimisha hata upate wokovu wa kweli uliojengwa juu ya Neno, sio juu ya hisia na misisimko (2 Tim. 2:15; 2 Tim. 3:15-17).
Ndugu Mpendwa hakika tuko katika Pambano NGUVU mbili zinavutana inayokuongoza kujifunza neno nyingine inakuzuia ,rafiki wewe kama wewe sio rahisi kuishinda hii vita mpaka umruhusu YESU aongoze maisha yako .Unaweza ukashuhudia upinzani uliopo unapotaka kusoma neno la Mungu ila kwa uweza wake atakuongoza utalielewa usikate tamaa .
Mungu akubariki unapoendelea kujifunza neno lake.Karibu kwa sura ya 11.

ConversionConversion EmoticonEmoticon