MAFUNDISHO YA UONGO YALIVYOINGIA

Ninachukua hii nafasi kukuarika tena mpendwa na rafiki katika kujifunza neno la Mungu ,ukiangalia kwa umakini hata sasa kuna mambo mengi yanayoendelea hapa duniani ,ukiangalia kila kukicha mambo mapya mengi yanaibuka rafiki usishangae hata tukio la hivi karibuni juu ya raisi wa marekani kuutambua yerusalemu kama mji mkuu ya israeli haya yote hayatokei bila kuwa katika mpango au kujurikana hapo awali ,mambo yote yanayofanyika hayafanyiki kwa bahati mbaya bali yako katika mpangilio ,ueipate shaka nitakuletea matukio ya siku hizi kwa uwazi kabisa ,karibu kwa masomo haya ,
Mgunduzi wa Mafundisho ya Uongo ni shetani ,hapo awali Shetani  alijua  fika  ya  kwamba  Maandiko  yale  Matakatifu yangewawezesha  wanadamu  kuyang’amua  madanganyo  yake  na kuupinga  uwezo  wake.  
Ilikuwa  ni  kwa  njia  ya  Neno  hilo  hata yule  Mwokozi  wa  ulimwengu  aliweza  kuyapinga  mashambulio yake.   Kwa  kila  shambulio  lake  [Shetani],  Kristo  alionyesha ngao  ya  ile  kweli  ya  milele,  akisema,  “Imeandikwa.”   Kwa  kila shauri  alilotoa  yule  adui,  alikataa  kwa  kutegemea  hekima  na uwezo  wa  lile  neno.   Ili  huyo  Shetani  apate  kudumisha  utawala wake  juu  ya  wanadamu,  na  kuimarisha  mamlaka  ya  tapeli  yule wa  kipapa,  ilikuwa  ni  lazima  kwake  kuwaweka  watu  katika  hali ya  ujinga  wa  kutoyajua  Maandiko.   Biblia  ingemtukuza  Mungu na  kuwaweka  wanadamu  mahali  pao  panapowastahili  hasa;   kwa hiyo  ilikuwa  ni  lazima  kwamba  zile  kweli  zake  takatifu  zifichwe kwa  watu  na  kupigwa  marufuku.   Mantiki  hiyo  ikatumiwa  na Kanisa  la  Roma.  
Kwa  mamia  ya  miaka  uenezaji  wa  Biblia ulipigwa  marufuku.   Watu  walikatazwa  kuisoma  au  kuwa  nayo katika  nyumba  zao,  na  makasisi  (mapadre)  pamoja  na  maaskofu wapotovu  wakayafafanua  mafundisho  yake  ili  yapate  kuunga mkono  unafiki  wao.  Hivyo  ndivyo  papa  alivyokuja kutambulikana  karibu  ulimwenguni  kote  kama  Kaimu  wa  [Aliye Badala  ya]  Mungu  hapa  duniani,  ambaye  alipewa  mamlaka  juu ya kanisa na serikali.Kuupigia Magoti Upagani Baada  ya  kuondolewa  yule  anayegundua  mafundisho potofu  [yaani,  Biblia],  Shetani  akafanya  kama  apendavyo. Unabii  ulikuwa  umetangaza  kwamba  upapa  unge“azimu kubadili  majira  na  Sheria  [Amri  Kumi].”   Danieli  7:25.   Kazi hiyo  [upapa]  haukuchelewa  kuanza  kuifanya.   Ili  kuwapa waongofu  waliotoka  kwenye  upagani  kitu  fulani  badala  ya  ibada yao  ya  sanamu,  na  kukuzia  upokeaji  wao  wa  Ukristo  kwa  jina  tu, kuabudu  sanamu  na  mabaki  ya  mifupa  ya  watakatifu  waliokufa zamani  vikaingizwa  taratibu  katika  ibada  ya  Kikristo.   Amri iliyotolewa  na  baraza  kuu  hatimaye  ikauimarisha  mfumo  huo  wa ibada  ya  sanamu.   Kuikamilisha  kazi  hiyo  ya  kukufuru,  Roma ikadhamiria  kuifutilia  mbali  kutoka  katika  Sheria  ya  Mungu [Amri  Kumi]  amri  ile  ya  pili  inayokataza  ibada  ya  sanamu,  na kuigawa  amri  ile  ya  kumi  ili  kuhifadhi  idadi  ile  ile  [ya  Amri Kumi]

SHERIA YA MUNGU

I -Usiwe na miungu mingine ila mimi.

II -Usijifanyie  sanamu  ya  kuchonga,  wala mfano  wa  kitu  cho  chote  kilicho  juu Mbinguni,  wala  kilicho  chini  duniani, wala  kilicho  majini  chini  ya  dunia. Usivisujudu  wala  kuvitumikia;   kwa kuwa  mimi,  BWANA,  Mungu  wako,  ni Mungu  mwenye  wivu;   nawapatiliza wana  maovu  ya  baba  zao,  hata  kizazi cha  tatu  na  cha  nne  cha  wanichukiao, nami  nawarehemu  maelfu  elfu Wanipendao, na kuzishika amri zangu.

III -Usilitaje  bure  jina  la  BWANA,  Mungu wako,  maana  BWANA  hatamhesabia kuwa  hana  hatia  mtu  alitajaye  jina  lake bure.

 IV -Ikumbuke  siku  ya  Sabato  uitakase.   Siku sita  fanya  kazi,  utende  mambo  yako yote;  Lakini  siku  ya  saba  ni  Sabato  ya BWANA,  Mungu  wako,  siku  hiyo usifanye  kazi  yo  yote,  wewe,  wala mwana  wako,  wala  binti  yako,  wala mtumwa  wako,  wala  mjakazi  wako, wala  mnyama  wako  wa  kufuga,  wala mgeni  aliye  ndani  ya  malango  yako. Maana,  kwa  siku  sita  BWANA  alifanya Mbingu,  na  nchi,  na  bahari,  na  vyote vilivyomo,  akastarehe  siku  ya  saba; Kwa  hiyo  BWANA  akaibarikia  siku  ya Sabato akaitakasa.

 V -Waheshimu  baba  yako  na  mama  yako; siku  zako  zipate  kuwa  nyingi  katika  nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

VI- Usiue.

VII- Usizini.

VIII -Usiibe.

 IX -Usimshuhudie jirani yako uongo.

X- Usiitamani  nyumba  ya  jirani  yako, usimtamani  mke  wa  jirani  yako, mtumwa  wake,  wala  mjakazi  ,  wala ng’ombe  wake,  wala  punda  wake,  wala cho chote alicho nacho jirani yako. Kutoka 20:3-17

SHERIA YA MUNGU KAMA ILIVYOBADILISHWA NA MWANADAMU

I - Mimi  ni  Bwana  Mungu  wako, Usiwe  na  miungu  migeni  ila  mimi. (Amri  ya  Pili  Imeachwa.)

II- (Hii  hasa  ni  ya  III) Usilitaje  bure  jina  la  Bwana,  Mungu  wako.

 III- (Hii  hasa  ni  ya  IV) Kumbuka  kwamba unaitakasa  siku  ya  Sabato. (Amri  ya  Sabato  imebadilishwa  vibaya  sana!)

IV- (Hii  hasa  ni  ya  V) Waheshimu  baba  na  mama  yako.

 V- (Hii  hasa  ni  ya  VI) Usiue.

 VI- (Hii  hasa  ni  ya  VII)Usizini

 VII- (Hii  hasa  ni  ya  VIII) Usiibe.

VIII- (Hii  hasa  ni  ya  IX) Usimshuhudie  jirani  yako  uongo.

IX- (Hii  hasa  ni  ya  X,  Sehemu  ya  Kwanza) Usimtamani  mke  wa  jirani  yako.

X- (Hii  hasa  ni  ya  X,  Sehemu  ya  Pili) Usitamani  mali  ya  jirani  yako.
Katekisimu ya Wote ya Kikatoliki

Maridhiano Yaendelea


 Roho  ile  ya  maridhiano  na  upagani  ikafungua  njia  ya kutoijali  sana  Mamlaka  ile  ya  Mbinguni.  
Shetani,  akifanya  kazi yake  kwa  kuwatumia  viongozi  wa  kanisa  wasiojitoa  wakf  kwa Mungu,  akaigeuza  amri  ile  ya  nne  pia,  na  kujaribu  kuiweka kando  Sabato  ile  ya  kale  [Jumamosi],  siku  ambayo  Mungu alikuwa  ameibarikia  na  kuitakasa,  na  mahali  pake  kuitukuza sikukuu  iliyoadhimishwa  na  makafiri  kama  “siku  tukufu  ya  jua” [Jumapili].  
 Badiliko  hilo  mwanzoni  halikufanywa  waziwazi.
Katika  karne  zile  za  mwanzo  Sabato  ya  kweli  [Jumamosi] ilikuwa  imetunzwa  na  Wakristo  wote.   Walikuwa  na  wivu  kwa ajili  ya  heshima  ya  Mungu,  na,  wao  wakiwa  wanaamini  kwamba Sheria  ya  Mungu  [Amri  Kumi]  haibadiliki  kamwe,  basi,  kwa bidii  nyingi  walitunza  utakatifu  wa  amri  zake  [kumi].  
 Lakini kwa  usiri  mkubwa  Shetani  alifanya  kazi  yake  kupitia  kwa vibaraka  wake  ili  kutekeleza  lengo  lake.   Ili  mawazo  ya  watu yapate  kugeuzwa  kuelekea  kwenye  ile  Jumapili,  ikafanywa kuwa  sikukuu  ya  kuheshimu  ufufuo  wa  Kristo.  
 Ibada  za  dini zikaendeshwa  kataika  siku  hiyo;   lakini  bado  ilifikiriwa  kama siku  ya  mapumziko  tu,  Sabato  [Jumamosi]  ikiwa  inaendelea kutakaswa.

 Kutayarisha  njia  kwa  ajili  ya  kazi  ile  aliyokusudia kuifanya,

  Shetani  akawaongoza  Wayahudi,  kabla  ya  kuja  kwa Kristo,  kuiwekea  Sabato  mizigo  mizito  na  masharti  makali, wakifanya  utunzaji  wake  kuwa  mzigo  mzito  ulemeao.
  Basi, [Shetani]  akiitumia  nafasi  hiyo  ya  kuwapo  kwa  nuru  ile  ya uongo  ambayo  kwayo  aliifanya  [Sabato]  ifikiriwe  vibaya, akaifanya  ipate  kudharauliwa  na  watu  kama  siku  ya  Wayahudi, Wakati  Wakristo  wakiendelea  kwa  kawaida  kuiadhimisha Jumapili  kama  sikukuu  ya  furaha,  akawaongoza  kuifanya  siku ya  Sabato  [Jumamosi]  kuwa  siku  ya  kufunga  [saumu],  yaani, siku  ya  huzuni  na  majonzi,  ili  kuonyesha  chuki  yao  dhidi  ya  dini ile ya Kiyahudi

Badiliko la Kijasiri

Katika  sehemu  ile  ya  kwanza  ya  karne  ya  nne  mfalme Konstantino  alitoa  amri  na  kuifanya  Jumapili  kuwa  sikukuu  ya serikali  katika  dola  yote  ya  Waroma.   Siku  hiyo  ya  jua [Jumapili]  iliheshimiwa  na  raia  zake  wapagani,  tena iliheshimiwa  na  Wakristo;   ilikuwa  ni  sera  ya  mfalme  yule kuunganisha  mambo  yale  waliyoyapenda  makafiri  na  Wakristo ambayo  yalikuwa  yanaleta  mgongano.   Alishurutishwa  kufanya hivyo  na  maaskofu  wa  kanisa,  wakiwa  wamechochewa  na  tamaa ya  ukuu  na  kiu  ya  mamlaka  walitambua  kwamba  kama  siku  ile ile  moja  ingeadhimishwa  na  Wakristo  na  makafiri,  basi, ingeweza  kusaidia  kupokelewa  kwa  Ukristo  na  wapagani  wale na  kwa  njia  hiyo  kuendeleza  mbele  mamlaka  na  utukufu  wa kanisa.  
Lakini  Wakristo  wengi  wacha  Mungu waliposhawishiwa  polepole  kuifikiria  Jumapili  kama  ina kiwango  fulani  cha  utakatifu,  bado  waliendelea  kuitunza  Sabato ya  kweli  [Jumamosi]  kama  takatifu  kwa  Bwana,  tena  waliitunza kwa kutii amri ile ya nne [Kut. 20:8-11].

Laghai  yule  mkuu  [Shetani]  alikuwa  bado  hajaikamilisha kazi  yake.   Akaazimu  kuukusanya  pamoja  Ulimwengu  wote  wa Kikristo  chini  ya  bendera  yake  na  kutumia  uwezo  wake  kupitia kwa  kaimu  wake,  yaani,  yule  papa,  mwenye  majivuno  mengi, aliyejidai  kwamba  alikuwa  ndiye  mwakilishi  wake  Kristo.

 Kupitia  kwa  wapagani  wale  walioongoka  nusu-nusu,  na  kwa maaskofu  wale  wenye  kutaka  makuu,  na  kwa  watu  wa  kanisa walioipenda  dunia  akalitimiza  kusudi  lake.
  Mabaraza  makubwa sana yakafanywa  toka  wakati  hata  wakati,  na  katika  hayo viongozi  wakuu  wa  kanisa  walikutana  kutoka  pande  zote za ulimwengu.   Karibu  katika  kila  baraza  lililokaa,  Sabato [Jumamosi]  ambayo  Mungu  alikuwa  ameianzisha  ikasukumiwa chini  kidogo  zaidi,  wakati  ule  ule  Jumapili  ikawa  inainuliwa  juu.

 Hivyo  ndivyo  sikukuu  ile  ya  kipagani  [Jumapili]  ilivyokuja kuheshimiwa  hatimaye  kama  siku  iliyowekwa  na  Mungu,  na wakati  ule  ule  Sabato  ile  ya  Biblia  [Jumamosi]  ikatangazwa kuwa  ilikuwa  ni  mabaki  ya  dini  ile  ya  Kiyahudi,  na  watunzaji wake wakatangazwa kuwa wamelaaniwa.

Soma hii rejea

"Jumapili  imewekwa  na  Wakatoliki,  na  madai ya  kutaka  itunzwe  yanaweza  tu  kutetewa  kwa kufuata  kanuni  za  Kikatoliki….Toka  mwanzo hadi  mwisho  wa  Maandiko  Matakatifu  hakuna kifungu  hata  kimoja  kinachotoa  kibali  cha kuhamisha  ibada  ya  kila  juma  kutoka  katika siku  ile  ya  mwisho  wa  juma  kwenda  ile  ya kwanza."  Catholic  Press,   Sydney,  Australia, Agosti,  1900.

Muhuri wa Muumbaji Waondolewa

Mwasi  huyo  mkuu  alikuwa  amefanikiwa  kujiinua mwenyewe  “juu  ya  kila  kiitwacho  Mungu  ama  kuabudiwa.”   2 Wathesalonike  2:4.   Akadiriki  kuibadili  amri  ile  ya  pekee  katika Sheria  ya  Mungu  [Amri  Kumi]  ambayo  bila  kukosea  hata kidogo  inawaelekeza  wanadamu  wote  kwa  Mungu  wa  kweli, aliye  hai.  Katika  amri  ile  ya  nne  [Kut.  20:8-11]
 Mungu anadhihirishwa  kama  ndiye  Muumbaji  wa  mbingu  na  nchi,  na kwa  sababu  hiyo  yeye  anatofautishwa  na  miungu  yote  ya  uongo.
 Ilikuwa  ni  kwa  ajili  ya  kumbukumbu  ya  kazi  ile  ya  uumbaji, ndiyo  maana  siku  ile  ya  saba  [Jumamosi]  ilitakaswa  [ilitengwa kwa  matumizi  matakatifu]  kama  siku  ya  mapumziko  kwa  kila mwanadamu.   Ilikusudiwa  kumweka  Mungu  aliye  hai  daima kataika  mawazo  ya  wanadamu  kama  chimbuko  la  uhai  wao  na lengo  la  kicho  chao  na  ibada  yao.  
Shetani  anajitahidi  sana iuwageuza  watu  waache  kumtii  Mungu,  na  kuacha  kutoa  utii wao  kwa  Sheria  yake  [Amri  Kumi];   kwa  hiyo,  juhudi  zake anazielekeza  hasa  dhidi  ya  amri  ile  [ya  Sabato] inayomwonyesha Mungu kuwa ni Muumbaji. Waprotestanti  siku  hizi  wanasisitiza  kwamba  ufufuo wake  Kristo  katika  siku  ile  ya  Jumapili  ndio  ulioifanya  siku  hiyo kuwa  Sabato  ya  Kikristo.   Lakini  ushahidi  wa  Maandiko unakosekana.   Hakuna  heshima  kama  hiyo  iliyotolewa  kwa  siku hiyo [ya Jumapili] na Kristo au na Mitume wake.kiukweli Hakuna hiyo rejea kimaandiko bali hutumia kigezo cha kufufuka kwa Kristo ,ndugu rafiki ukweli huweka huru ,yohana 17:17 hufungua kutoka madhakani ,ninakuarika uendelee kufuatilia haya masomo na mengine yapo tayari katika hii blogspot waweza kujifunza zaidi, lakini ninakuomba usichoke kujifunza neno la Mungu yeye atakuongoza katika hii kweli ,daima omba zaidi ,soma neno kisha jitoe kumfuata hautapungukiwa hata kuurithi uzima wa milele ,Mungu akubariki Karibu kwa somo linalofuata .
Previous
Next Post »