PATAKATIFU SEHEMU YA PILI

Ndugu mpendwa huu ni muendelezo wa somo la patakatifu waweza kusoma somo la nyuma kupitia hii blog shuka chini utaona sehemu ya preveous hapo utayakuta ya nyuma yote.karibu tunapoendelea

Siku Kuu ya Upatanisho Kuhani  mkuu  aliingia  katika  patakatifu  mno  mara  moja  kwa  mwaka ili  kutakasa  patakatifu.    

Je mambo yalikuwaje wakati ule

Mbuzi  wawili waliletwa  na  kupigiwa  kura.  
 Kura  moja kwa  Bwana  na  kura  moja  kwa  Azazeli.
 Mbuzi  wa  Bwana  alichinjwa  kama  sadaka  ya  dhambi  kwa  ajili  ya  watu.    Na kuhani  alichukua  damu  akaingia  patakatifu  mno,  akainyunyiza  kwenye  kiti cha  rehema  na  juu  ya  madhabahu  ya uvumba.    “Na  haruni  ataweka  mikono yake  miwili  juu  ya  kichwa  cha  yule mbuzi  aliye  hai,  na  kuungama  juu  yake uovu  wote  wa  wana  wa  Israeli,  na  makosa  yao,  naam,  dhambi  zao  zote;  naye ataziweka  juu  ya  kichwa  chake  yule mbuzi,  kisha  atampeleka  aende  jangwani  kwa  mkono  wa  mtu  aliye  tayari.
 Na  yule  mbuzi  atachukua  juu  yake uovu  wao  wote,  mpaka  nchi  isiyo  watu;  naye  atamwacha  mbuzi  jangwani.”  Law. 16:21-22. Huduma  hiyo  ilikusudiwa  kuwaonyesha  Waisraeli  utakatifu  wa  Mungu,  na jinsi  anavyoichukia  dhambi.  

  Kila  mtu alitakiwa  kujitakasa  kwa  njia  ya  kujichunguza  wakati  huduma  hii  inapokuwa ikiendeshwa.    
Kazi  zote  na  shughuli  ziliachwa  kabisa,  na  Waisraeli  walitumia siku  hiyo  katika  ibada  na  maombi,  haliwakifunga  na  kujipeleleza  mioyo  yao  na kuungama. Damu  ya  kafara  ilikubaliwa  badala  ya mwenye  dhambi  kufa,  lakini  hatia  ya dhambi  haikufutwa  kwa  njia  ya  damu ya  mnyama,  ila  ilihamishwa  mpaka  katika  patakatifu.    

Kule  kutoa  damu  mwenye  dhambi  alikiri  madaraka  ya  sheria, akaungama  kuwa  amevunja  sheria,  na akaamini  na  kuonyesha  imani  juu  ya mkombozi  atakayekuja,  ambaye  anafananishwa  kwa  mfano  wa  huduma  hiyo.  Walakini  alikuwa  hajafunguliwa  kabisa atokane  na  hukumu  ya  kuvunja  sheria.  
 Siku  ya  upatanisho  kuhani  mkuu akiisha  kupokea  sadaka  ya  watu,  aliingia  patakatifu  mno.    Alinyunyiza  damu ya  sadaka  hiyo  juu  ya  kiti  cha  rehema moja  kwa  moja  kwenye  sheria,  ili  kuiridhisha  kwa  kule  kuvunjwa  kwake.  Halafu  kama  mwombezi  alizichukua dhambi  zote  juu  yake  kutoka  patakatifu.  

 Wakati  anapoweka  mikono  yake  juu ya  yule    mbuzi  wa  Azazeli  huzihamisha dhambi  hizo  na  kuziweka  juu  ya  mbuzi.  Basi  mbuzi  huzichukua  zote.    Ndipo kuhesabiwa  kana  kwamba  zimetoweka milele, kutoka kwa watu. Ukweli  wa  Mbinguni Yale  yaliyofanyika  katika  huduma  ya patakatifu  pa  duniani,  ambapo  palikuwa  kivuli  cha  yale  ya  mbinguni, ndivyo  yalifanyika  mbinguni  ambako ndiko  jambo  halisi,  katika  patakatifu pa  huko.    Mwokozi  wetu  baada  ya  kufufuka  kwake  na  kupaa  mbinguni  na kuanza  kazi  yake  kama  kuhani  Mkuu.
Kwa  sababu  Kristo    hakuingia  katika patakatifu  palipofanyika  kwa  mikono, ndio  mfano  wa  patakatifu  halisi;  bali aliingia  mbinguni  hasa,  aonekane  sasa usoni  pa  Mungu  kwa  ajili  yetu”.    Ebr.  9:24.

Huduma  ya  kuhani  iliyokuwa  ikifanyika  katika  chumba  cha  kwanza cha  patakatifu,  ni  mfano  wa  huduma ya  Kristo  iliyoanza  mbinguni  baada  ya kupaa  kwake.    Kuhani  katika  huduma yake  ya  kila  siku,  alileta  damu  ya  sadaka  mbele  za  Mungu,  ambayo  ni  sadaka  ya  dhambi,  pamoja  na  uvumba uliopaa  juu  pamoja  na  sala  za  watakatifu  (Waisraeli).    Vivyo  hivyo  Kristo  aliombea  damu  yake  mbele  za  Baba,  kwa  ajili ya  wenye  dhambi,  na  kuweka  harufu njema  ya  haki  yake  mwenyewe  mbele za  Baba,  sala  za  wenye  kutubu  makosa yao.    Hiyo  ilikuwa  huduma  iliyokuwa ikifanyika  katika  patakatifu,  katika mbingu.
Hapo  imani  ya  wanafunzi  ilimfuata  alipopaa  juu,  hapo  matumaini  yao yaliimarika,  “tumaini  tulilo  nalo  kama nanga  ya  rohoni,  ambalo  ni  la  hakika lililo  imara”    yaingiayo  hata  mle  mlimo ndani  ya  pazia,  alimoingia  Yesu  kwa  ajili yetu,  mtangulizi  wetu  amekuwa  Kuhani Mkuu  hata  milele.  

 “Wala  si  kwa  damu ya  mbuzi  na  ndama, bali  kwa damu yake mwenyewe  aliingia  mara  moja  tu  katika patakatifu,  akiisha  kupata  ukombozi wa milele”.  Ebr.  6:19-20; 9:12.

Kwa  muda  wa  karne  kumi  na  nane kazi  hiyo  imekuwa  ikifanyika  mbinguni  katika  chumba  cha  kwanza  cha  patakatifu.    Damu  ya  Kristo  imeleta  msamaha wa dhambi na kibali  cha  Baba  cha kuwakubali  wenye  kutubu.    Walakini dhambi  zao  bado  zingali  katika  vitabu.  Kama  katika  mfano  ulivyo,  kuna  siku ya  upatanisho  kwa  mwaka,  vivyo  hivyo kazi  ya  Kristo  kwa  ajili  ya  wanadamu haikamiliki  mpaka  kazi  ya  kulipa,  au kafara  ya  malipo  ifanyike.    Kazi  hiyo  ni ya  kuziondoa  dhambi  katika  patakatifu.
 Hii  ilianza  wakati  siku  2300  zilipomalizika.    Wakati  huo  Kuhani  wetu  Mkuu aliingia  katika  patakatifu  mno  ili  kutakasa patakatifu.
 Kazi ya Hukumu Katika  agano jipya  dhambi za watu wenye    kutubu  huwekwa  juu  ya  Kristo,  na kuhamishiwa  mpaka  katika  patakatifu pa  mbinguni.    Na  jinsi  ilivyokuwa  katika  patakatifu  pa  duniani,  dhambi  zilikuwa    zikiihamishwa  kutoka  patakatifu ili  kukamilisha  kazi,  hali  kadhalika  na kutakasa  patakatifu  pa  mbinguni  patakamilika  kwa  njia  hiyo  hiyo  ya  kuhamisha  dhambi  kutoka  vitabuni.  
 Kazi hii  itakuwa  kuangalia  vitabu  na  kupima  kuona  ni  nani  ametubu  kikweli  na kuwa  na  imani  kwa  Kristo,  ili  afaidike  kulipiwa  adhabu  yake  kwa  dhabihu  ya Kristo.    Kutakaswa  kwa  patakatifu  basi ni  kazi  ya  uchaguzi,  kazi  ya  hukumu, kuona  kuwa  ni  nani  anastahili  kupata uzima,  na  ni  nani  hastahili.  

 Kazi  hii  itafanyika  kabla  ya  kuja  kwa  Kristo.    Maana  ajapo  atakuja  na  ujira  wake  kumlipa kila  mtu  kama  kazi  yake  itakavyokuwa.  Ufunuo  22:12.
Hivyo  wale  waliofuata  unabii  unavyoelekeza,  waliona  kuwa  badala  ya Kristo  kuja  dunia  mwisho  wa  siku 2300,  yaani  mwaka  1844,  aliingia  katika  patakatifu  pa  patakatifu  mbinguni ili  kumaliza  kazi  yake  ya  uombezi  na malipo  ya  adhabu  kwa  ajili  ya  dhambi, kabla ya kuja kwake duniani.
Dhambi zime samehewa juu ya kondoo na kuwekwa juu yake na katika damu ambayo huhamishwa na kupelekwa hekaluni. Sasa Kristo huzipokea dhambi na kuzihamisha katika hekalu la mbinguni.
Kristo  akimaliza  kuondoa  dhambi  za watu  wake  kutoka  patakatifu  pa  mbinguni  mwishoni  mwa  kazi  yake  ataziweka  zote  juu  ya  Shetani,  atakayepata adhabu ya mwisho. Mbuzi  wa  Azazeli  alipelekwa  porini  na kuachwa  huko.    

Hali  kadhalika  Shetani  naye  atatengwa  mbali  na  Mungu milele,  wala  asionekane  tena,  kwa  watu wa  Mungu.    Naye  ataangamizwa  kabisa,  wala  hatasalia  na  aina  yoyote  ya kumbukumbu.    Wakati  huo  dhambi  pia na  wenye  dhambi  pia  wataangamizwa milele.ndugu Mpendwa na rafiki katika Kristo ninakukaribisha katika kujitoa tungali bado katika kipindi hiki ,kabla YESU hajarudi kwa Mara ya pili atukute tuko tayari tukimngoja kama Bwana na mkombozi wetu .

Karibu sana tunapoendelea na sehemu inayofuata hasa katika unabii wa kitabu cha ufunuo.
Mungu akubariki sana.
Previous
Next Post »