Toka Roma ya Kipagani Kwenda Roma ya Kipapa
Katika karne ile ya sita upapa ulikuwa umejiimarisha sana. Kiti chake cha enzi kilikuwa katika mji ule wa dola [Roma], na Askofu wa Roma [Papa] akatangazwa kuwa ndiye kichwa cha kanisa lote. Upagani ukaupa upapa nafasi yake [Dan. 8:12; 12:11]. Yule Joka [Ibilisi na Roma ya Kipagani Ufu. 12:9,3] alikuwa amempa mnyama [mfalme – Dan. 7:17] “nguvu zake na kiti chake cha enzi, na uwezo mwingi.” Ufunuo 13:2. Na sasa ikaanza ile miaka 1260 ya mateso [mauaji] ya papa yaliyokuwa yametabiriwa katika unabii wa Danieli na Ufunuo. Danieli 7:25; Ufunuo 13:5-7. Wakristo wakalazimishwa ama kuuacha msimamo wao mnyofu na kuzikubali sherehe za kipapa pamoja na ibada yake, ama kuchomwa moto juu ya kitita cha kuni, ama kukabiliwa na mtu yule akataye vichwa kwa shoka. Basi, maneno ya Yesu yakawa yametimizwa, aliyosema: “Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha [watawaua] baadhi yenu. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.” Luka 21:16,17. Mateso yakaanzishwa rasmi dhidi ya wale waliokuwa waaminifu kwa ukali sana kuliko wakati wo wote uliopita, na dunia hii ikawa ni uwanja mkubwa wa vita. Kwa mamia ya miaka Kanisa la Kristo likapata kimbilio lake katika maeneo ya upweke na ya siri. Nabii yule asema hivi: “Yule mwanamke [Kanisa la Kristo la Kweli] akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko kwa muda wa siku [miaka – Eze. 4:6] elfu na mia mbili na sitini.” Ufunuo 12:6ZAMA ZA GIZA ZAANZA Kule kujipatia mamlaka yake lile Kanisa la Roma ndio mwanzo wa Zama za Giza. Kadiri uwezo wake ulivyozidi kuongezeka, ndivyo giza [yaani, ujinga wa kutoijua Biblia, Sayansi na Teknolojia] lilivyozidi kuwa nene. Imani ikahamishwa kutoka kwa Kristo, aliye msingi wa kweli, kwenda kwa papa wa Roma. Badala ya kumtegemea Mwana wa Mungu kwa msamaha wa dhambi na wokovu ule wa milele, watu wakamtazama papa, na makasisi (mapadre) na maaskofu ambao alikuwa amewakabidhi mamlaka. Wakafundishwa ya kwamba papa alikuwa ndiye mpatanishi wao wa kibinadamu na ya kwamba hakuna hata mmoja ambaye angeweza kumwendea Mungu isipokuwa kwa kupitia kwake, na kwa ajili hiyo yeye alipaswa kupewa utii bila swali lo lote. Kwenda kinyume na matakwa yake ilikuwa ni sababu ya kutosha ya kutolewa adhabu kali sana juu ya miili na roho za wale wahalifu. Kwa njia hiyo, mawazo ya watu yakageuziwa mbali na Mungu na kuelekezwa kwa wanadamu wawezao kukosa, kupotoka, na wakatili, naam, zaidi sana, kwa yule mkuu wa giza mwenyewe [Shetani], ambaye alitumia uwezo wake kupitia kwa watu wale. Dhambi ikafichwa katika vazi la utakatifu. Maandiko yanapozuiwa kusomwa na watu, na mwanadamu anapokuja kujiona mwenyewe kuwa ni mkubwa kuliko wote, hapo ndipo tunapohitaji tu kutazamia kuona hila, udanganyifu, na uovu unaoishusha hadhi ya mwanadamu. Katika kuzitukuza sheria za wanadamu na mapokeo ukaonekana ufisadi ambao hutokea daima wakati Sheria ya Mungu [Amri Kumi] inapowekwa kando.Siku za Hatari Kubwa Kristo. Zile zilikuwa ni siku za hatari kubwa kwa Kanisa lake Waaminifu walioibeba bendera yake walikuwa ni wachache kweli kweli. Ingawa ile kweli haikuachwa bila kuwapo mashahidi, hata hivyo, wakati fulani ilionekana kana kwamba mafundisho yale ya uongo na ushirikina yalikuwa yameenea kote, na dini ile ya kweli ilionekana kana kwamba ingeweza kufutiliwa mbali duniani kote. Injili ikawa imesahauliwa, lakini mitindo ya dini ikaongezeka, na watu wakawa wamelemewa na mizigo mizito waliyotwishwa yenye masharti makali. Wakafundishwa sio tu kumtazama papa kama ndiye mpatanishi wao, bali kutegemea matendo yao wenyewe ili kuweza kulipa fidia ya dhambi zao. Safari ndefu za taabu kwenda kuzuru patakatifu, kutenda matendo ya kitubio, kuabudu mifupa ya watakatifu waliokufa zamani, kujenga makanisa, kujenga makaburi ya watakatifu, na altare [madhabahu], kulipa fedha nyingi kwa kanisa - mambo hayo pamoja na matendo mengine yanayofanana na hayo yaliamriwa ili kuituliza ghadhabu ya Mungu au kupata upendeleo wake, kana kwamba Mungu alikuwa kama wanadamu, kuweza kukasirishwa kwa mambo madogo sana yasiyo na maana, au kutulizwa kwa kupewa zawadi au kwa maungamo (kitubio)! Giza lile likaonekana kana kwamba lilikuwa likiongezeka kuwa nene zaidi. Ibada ya sanamu ikawa ni la kawaida kwa watu wengi. Mishumaa ikawashwa mbele ya sanamu zile na sala zikatolewa kwa sanamu zile. Desturi zile za kipuuzi kabisa na za kishirikina, hata akili zao zenyewe zikaonekana kana kwamba zimepoteza uwezo wake wa kujitawala. Wakati wale makasisi (mapadre) na maaskofu wenyewe walikuwa wanapenda anasa, uasherati, na ufisadi, iliweza kutazamiwa tu kwamba, watu wale waliowategemea kwa uongozi wao, nao wangeweza kuzama katika ujinga na uovu wao.Papa yule Mwenye Majivuno Hatua nyingine katika dhana za kipapa ilichukuliwa katika karne ile ya kumi na moja wakati Papa Gregori wa Saba alipotangaza ukamilifu wa Kanisa la Roma. Miongoni mwa mawazo yake aliyotoa lilikuwapo wazo moja lililosema kwamba kanisa lile [la Roma] lilikuwa halijapata kukosea kamwe kulingana na Maandiko. Lakini ushuhuda wa Maandiko hayo haukuambaatana na lile dai lake. Papa yule mwenye majivuno mengi alidai pia kwamba anao uwezo wa kuwaondoa wafalme katika kiti chao cha enzi, kisha akatangaza kwamba hakuna hukumu yo yote aliyoitoa yeye ambayo ingeweza kubatilishwa [kugeuzwa] na mtu ye yote, ila kwamba yeye ndiye alikuwa na haki ya kuyabatilisha [kuyageuza] maamuzi ya wengine wote. Ni tofauti kubwa ya kushangaza mno jinsi gani kati ya kiburi kile kilichojaa uonevu cha papa yule mwenye majivuno mengi ukilinganisha na upole na unyenyekevu wa moyo aliokuwa nao Kristo, ambaye anajiwakilisha mwenyewe kama mmoja anayebisha katika mlango wa moyo akiomba kuingia ndani, ili apate kuingia humo na kuleta msamaha na amani, na ambaye aliwafundisha wanafunzi wake, akasema: “Na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu.” Mathayo 20:27.Giza Lazidi Kuwa Nene Karne zile zilipozidi kusonga mbele zilishuhudia ongezeko la daima la uongo katika mafundisho ya dini yaliyotolewa kutoka Roma. Hata kabla ya kuanzishwa kwa upapa mafundisho ya wanafalsafa wale makafiri yalikuwa yamezingatiwa, nayo yalitoa mvuto wake ndani ya kanisa. Wengi waliodai kwamba wameongoka walikuwa bado wanazing'ang'ania itikadi za falsafa yao ya kipagani, na si kwamba tu waliendelea kujifunza falsafa hiyo wao wenyewe, bali waliwashurutisha wengine kuipokea kama njia ya kueneza mvuto wao miongoni mwa makafiri wale. Makosa mazito yakaingizwa kwa njia hiyo katika imani ya Kikristo. Lililojitokeza sana katika hayo ni ile imani kwamba mwanadamu ana roho isiyokufa, na ya kwamba, akifa bado anaendelea kuwa na fahamu zake. Fundisho hilo la dini likaweka msingi ambao juu yake Roma ilianzisha sala kwa ajili ya watakatifu waliokufa na ibada ya Bikira Maria. Kutokana na fundisho hilo pia ukazuka uzushi uliosema kwamba wale ambao hatimaye hawataweza kutubu wataendelea kuteswa motoni milele hata milele, fundisho ambalo liliingizwa katika imani ya kipapa.Ndipo njia ikawa imetayarishwa ya kuingizwa [kanisani] mavumbuzi mengine ya kipagani ambayo Roma iliyaita kwa jina la 'Toharani' (purgatory), nao wakalitumia fundisho hilo kuwatisha makundi ya watu wale waliokuwa wajinga na washirikina. Kwa uzushi wao huo, wanathibitisha kwamba pako mahali pa mateso, ambapo roho za wale wasiostahili adhabu ya milele zinapaswa kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, na ya kwamba, kutoka hapo, zinapowekwa huru mbali na uchafu wake, roho hizo huingizwa mbinguni.
Mtazamo wa Kifedha Bado ikawapo haja ya kubuni uongo mwingine ili kuiwezesha Roma kunufaika kutokana na hofu hiyo na maovu ya wafuasi wake. Uongo huo uliwezekana kwa fundisho lao la indulgensia [ondoleo la dhambi]. Ondoleo kamili la dhambi, zilizopita, za sasa, na za baadaye, na kuachiliwa ili mtu asiweze kupatikana na maumivu yote pamoja na adhabu anazostahili [toharani], wakawa wameahidiwa kupewa wale wote ambao wangejiandikisha katika vita vya papa ili kupanua mipaka ya utawala wake wa kidunia, ili kuwaadhibu maadui zake, au kuwaangamiza kabisa wale ambao wangethubutu kuupinga ukuu wake usio na kifani. Watu walifundishwa pia kwamba kwa kulipa fedha kwa kanisa wangeweza kujiweka huru mbali na dhambi, na pia kuzifungua roho za marafiki zao waliokufa zilizokuwa zimefungiwa katika moto ule wa mateso. Kwa njia kama hizo Roma ilijaza makasha yake kwa fedha na kuendeleza ufahari, anasa, na uovu wa wale wawakilishi wanafiki wa yeye [Kristo], ambaye hakuwa na mahali pa kulaza kichwa chake. "Papa si mwakilishi tu wa Yesu Kristo, bali yeye ndiye Yesu Kristo, aliyejificha katika vazi la mwili." The Catholic National, Julai 1895.Muumbaji Aumbwa Agizo la Maandiko kuhusu Meza ya Bwana lilikuwa limeondolewa na mahali pake ikawekwa ibada ya sanamu ya Misa. Makasisi (mapadre) wa kikatoliki, kwaa kutamka maneno fulani ya kidini yasiyo na maana, wakajifanya kuwa wanaweza kuugeuza mkate wa kawaida na divai kuwa "mwili na damu [halisi] ya Kristo." - Kadinali Wiseman, The Real Presence of the Body and Blood of Our Lord Jesus Christ in the Blessed Eucharist, Provede From Scripture, hotuba ya 8, Sehemu ya 3, aya ya 26. Kwa kiburi chao cha makusudi kabisa kilichojaa makufuru, walidai waziwazi kwamba wanao uwezo wa kumwumba Mungu, Muumbaji wa vitu vyote. Wakristo walitakiwa, kwa tishio la kifo, kukiri imani yao katika uzushi huo wa kutisha unaoitukanisha Mbingu. Watu wengi waliokataa walitupwa motoni.
Mamilioni ya Wafiadini Katika karne ile ya kumi na tatu kilianzishwa chombo cha papa cha kutisha mno, - yaani, ile Inkwizisheni [Mahakama ya Kanisa Katoliki ya kukomesha uasi]. Mkuu yule wa giza alifanya kazi yake pamoja na viongozi wa utawala huo msonge wa kipapa. Katika mabaraza yao ya siri Shetani na malaika zake waliyatawala mawazo ya watu wale waovu, ijapokuwa alikuwa haonekani kwa macho, malaika wa Mungu alikuwa amesimama katikati yao, akichukua kumbukumbu ya kutisha ya amri zao zilizojaa uovu na kuandika historia ya matendo yao ya kutisha mno kuweza kuonwa kwa macho ya kibinadamu. "Babeli Mkuu" [Roma] alikuwa "amelewa na damu ya watakatifu." Miili ya mamilioni ya wafiadini iliyokuwa imeharibiwa vibaya ikamlilia Mungu ili apate kulipiza kisasi kwa mamlaka hiyo asi. "Papa Yohane Paulo II aliomba msamaha kwa ajili ya vita iliyopiganwa kule Ulaya kati ya Wakatoliki na Waprotestanti katika kipindi kile cha Upingaji wa Matengenezo ya Kanisa Counter-Reformation)." U. S. News and World Report, Julai 3, 1995.Taarifa za habari hii pamoja na habari nyingine zinazofanana na hii ni kukiri uwajibikaji kwa mauaji ya mamilioni ya wafiadini katika kipindi kile cha za Giza kwa kutumia njia ya mzunguko. Biblia inatabiri kwamba chini ya hali zile za dhiki zilizo mbele yetu hivi sasa, Upapa na wale wanaouunga mkono watatumia tena nguvu za dola (serikali) kuwadhibiti wale wasiokubaliana na mafundisho yao ya dini. ******* "Kwa kukiri imani iliyo kinyume na Kanisa la Roma, historia inaweka kumbukumbu ya wafiadini zaidi ya watu milioni mia moja." Brief Bible Readings, ukurasa 16. "Tarehe 24 Agosti, 1527, Wakatoliki wa Roma kule Ufaransa, kwa mpango uliokuwa umepangwa mapema chini ya uongozi wa Majesuti, waliwaua Waprotestanti 70,000 Katika kipindi cha miezi miwili. Papa alishangilia sana kusikia matokeo hayo yaliyofaulu." Western Watchman, Novemba, 21, 1912, (La Kikatoliki).
"Kwamba hilo Kanisa la Roma limemwaga damu nyingi sana isiyo na hatia kuliko taasisi nyingine yo yote iliyopata kuwako miongoni mwa binadamu, jambo hilo halitaweza kutiliwa mashaka yo yote na Mprotestanti ye yote aliye na ujuzi wa kutosha wa Historia…. Haiwezekani kabisa kuwa na dhana kamili ya idadi kubwa ya wahanga wake waliouawa ." W. E. H. Lecky, History of the Rise and Influence of the Spirit of Rationalism in Europe, gombo la 2, ukurasa 32, toleo la 1910. "Inakadiriwa … wastani wa mauaji ya kidini ya watu 40,000 kwa kila mwaka wa kuwako kwa Upapa." John Dowling, The History of Romanism, ukurasa 541-542. [Upapa ulitawala miaka 1260 kuanzia 538 B.K. hadi 1798 B.K. Kwa hiyo makadirio ya chini kabisa ya wafiadini waliouawa na Kanisa la Roma ni 1260 x 40,000 = 50,400,000.]

1 comments:
Click here for commentsndugu hizo mada unaweza kunitumia kwa WhatsApp ili niweze kusoma vzr
ConversionConversion EmoticonEmoticon