ONYO LA MWISHO WA DUNIA SEHEMU YA PILI

Baraza  hilo,  likiwa  ni  kiungo  chenye  nguvu  kuliko  vyote  cha Umoja  wa  Mataifa,  limefanya  mkutano  wake  katika  ngazi  yake ya juu kabisa.”   Birmingham News, Jan. 31, 1992. “Wale  miongoni  mwetu  walio  chini  ya  miaka  sabini angalau  wataona  ukiwekwa  msingi  wa  mfumo  huo  wa  serikali ya  ulimwengu  mpya.   Wale  miongoni  mwetu  walio  chini  ya miaka  arobaini  kwa  hakika  wataishi  chini  ya  mamlaka  ya  bunge, serikali,  na  sheria  yake,  pamoja  na  utawala  wake.
  Naam, washindani  hao  watatu  [George  Bush,  Papa  Yohane  Paulo  II,  na Mikhail  Gorbachev]   -   pamoja  na  wengine  wengi  zaidi  kando  ya hao,  kwa  kadiri  wakati  unavyosonga  mbele   -   wanaongea  juu  ya huo  Mpango  wa  Ulimwengu  Mpya  si  kama  kitu  kinachokuja kwenye  kona  iliyo  mbali  sana  ya  wakati,  bali  kama  kitu  kilicho karibu sana kutokea.”  M. Martin,  Keys of This Blood, uk. 15-16. “Hiyo  ndiyo  ndoto  juu  ya  Mpango  huo.
  Kama  yalivyo mawazo  mengi  ya  kimapinduzi,  Ulaya  Iliyoungana  Pamoja  si wazo  jipya,  bali  ni  la  zamani  ambalo  limefufuliwa  tena.   Ndoto hiyo  ya  kuwapo  kwa  mpango  huo  na  umoja  ambayo  zamani ilikuwamo  katika  Roma  ile  ya  Makaisari,  iliendelea  kuwako kupitia  katika  kipindi  kile  cha  Zama  za  Kati  (kipindi  kiitwacho Zama  za  Giza  kwa  usahihi)  sio  tu  katika  Kanisa  la  Katoliki  la Roma,  bali  katika  ile  Dola  Takatifu  ya  Roma.”   Time,  Okt.  6, 1961. “Kile  kilichoundwa  chini  ya  Mkataba  wa  Roma  katika Soko  lao  la  Pamoja  ni  urasimu  mpya  uliounganishwa  kikiki, uliowekwa  kikiki  chini  ya  makao  makuu,  unaoongozwa  kikiki, unaotawaliwa  kikiki,  ambao  kwa  dhahiri  unajaribu  kuurejesha tena  kule  Ulaya  ule  mfumo  wa  uchumi  uliokuwako  katika  ile Dola  Takatifu  ya  Roma.”   Christian  Science  Monitor,  1962.
Previous
Next Post »