Je, Roma Itatawala Ulimwengu Tena?
Hili ni swali ambalo kila mmoja wetu leo bila ushabiki wala ubishi imetupasa kurejea katika unabii ili tujue zaidi nini hasa ukweli ulivyo, hebu tuiangalie kidogo historia kwa ufupi hapa. KANISA LA MTAKATIFU PETRO, ROMA
Maridhiano ya Kufisha,
Mtume Paulo, katika Waraka wake wa Pili kwa Wathesalonike, alitabiri juu ya uasi mkuu ambao ungeleta matokeo ya kuianzisha mamlaka ile ya upapa. Alitangaza kwamba siku ile ya kuja Kristo isingeweza kuja, “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa mtu yule wa dhambi (kuasi), mwana wa uharibifu; yule Mpingamizi [Mpinga Kristo], ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu [kanisa] la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Tena, zaidi ya hayo, Mtume huyo anawaonya ndugu zake kwamba “ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wakorintho 2:3,4,7.
Hata katika kipindi kile cha mwanzo kabisa aliona yakiingia ndani ya kanisa mafundisho potofu ambayo yangetayarisha njia ya kujitokeza kwa upapa. Kidogo kidogo, mwanzoni kwa siri na kimya kimya, na baadaye kwa wazi zaidi, ikaongezeka nguvu yake na kuitawala mioyo ya wanadamu, ile “siri ya kuasi” ikaiendeleza mbele kazi yake kwa kutumia madanganyo na makufuru. Karibu bila kutambulikana kabisa desturi zile za kikafiri zikaingia ndani ya kanisa la Kikristo.
Roho ile ya maridhiano na kufanana-fanana [na dunia] ilizuiwa kwa wakati fulani kutokana na mateso makali ambayo kanisa lilistahimili chini ya wapagani.
Lakini mateso yale yalipokoma, na Ukristo ulipoingia katika mabaraza na majumba ya kifalme, ndipo kanisa lile lilipouweka kando unyenyekevu ule wa Kristo na Mitume wake na kujitwalia ufahari na kiburi cha makuhani na watawala wale wa kipagani; na mahali pa matakwa ya Mungu likaweka nadharia za wanadamu pamoja na desturi zao.
Kuongoka kwa jina tu kwa Konstantino, mapema katika karne ile ya nne, kulileta shangwe kubwa; na ulimwengu [upagani], ukiwa umevikwa joho la mfano wa haki, ukatembea na kuingia ndani ya kanisa.
Basi, kazi ile ya uharibifu ikasonga mbele kwa haraka sana. Upagani, wakati ukionekana kana kwamba umeshindwa kabisa, ukawa ndio mshindi.
Roho yake ikalitawala kanisa lile. Mafundisho yake ya dini, sherehe zake, na ushirikina wake vikaingizwa katika imani na ibada ya wale waliojidai kuwa ni wafuasi wake Kristo.
Mtu wa Dhambi Maridhiano hayo kati ya Upagani na Ukristo yalikuwa na matokeo ya kujitokeza kwa “mtu yule wa dhambi” (man of sin) ambaye alitabiriwa katika unabii huo kuwa atakuwa Mpingamizi [Mpinga Kristo], na ya kwamba atajiinua mwenyewe juu ya Mungu. Mfumo huo mkubwa kabisa wa dini ya uongo ni kazi kuu ya kilele ya uwezo wake Shetani - yaani, ni kielelezo bora kabisa cha kazi ile inayostahili kukumbukwa ambayo inatokana na juhudi zake [Shetani] za kujiketisha yeye mwenyewe juu ya kiti cha enzi ili kuitawala dunia hii kama apendavyo yeye.
Siku moja Shetani alijitahidi sana kufanya maridhiano na Kristo. Akaja kwa Mwana wa Mungu katika nyika ile ya majaribu, na kumwonyesha falme zote za dunia hii pamoja na utukufu wake, na kujitolea kumpa vyote mikononi mwake mradi tu akubali kwamba mkuu yule wa giza [Shetani] ndiye mwenye mamlaka yote. Kristo alimkemea mjaribu yule mwenye kiburi na kumlazimisha kuondoka pale.
Lakini Shetani anapata mafanikio makubwa sana anapoyaleta majaribu yale yale kwa mwanadamu. Ili kujipatia manufaa na heshima za ulimwengu huu, kanisa lile likatafuta upendeleo na kuungwa mkono na wakuu wa dunia hii; na kwa njia hiyo, likiwa limemkana Kristo, likashawishiwa kutoa utii wake kwa mwakilishi yule wa Shetani- yaani, kwa Askofu [Papa] yule wa Roma.
Msingi wa Fundisho Hilo la Uongo Ni mojawapo la mafundisho makuu ya dini ile ya Kiroma kwamba papa ni kichwa kinachoonekana kwa macho cha kanisa la ulimwengu mzima la Kristo, kwamba amepewa mamlaka ya juu kabisa juu ya maaskofu na wachungaji wote katika sehemu zote za dunia hii. Zaidi ya hayo, papa amepewa vyeo vya Mungu. Amepewa cheo cha “Bwana Mungu Papa,” tena ametangazwa kuwa hawezi kukosea kamwe. Anadai kwamba wanadamu wote wanapaswa kumsujudu yeye. Dai lile lile alilolisisitiza Shetani katika nyika ile ya majaribu bado linasisitizwa naye [papa] kupitia katika Kanisa la Roma, na idadi kubwa sana ya watu wako tayari kumsujudu yeye. “Tunashikilia hapa duniani mahali pa Mungu Mwenyezi." Papa Leo wa 13, Katika Barua yake ya Utume, Juni 20, 1894. Lakini wale wanaomcha na kumheshimu Mungu, kama vile Kristo alivyopambana na ubembelezi wa yule adui mwerevu, wanapambana na madai hayo yatokanayo na ushupavu wake wa kujinyakulia vyeo vya Mungu, wakisema: “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” Luka 4:8. Mungu hajatoa dokezo lo lote katika Neno lakelisemalo kwamba amemchagua mwanadamu fulani kuwa kichwa cha kanisa lake.
Fundisho la dini la ukuu wa papa usio na kifani hupingana moja kwa moja na mafundisho ya Maandiko. Papa hawezi kuwa na mamlaka yo yote juu ya Kanisa la Kristo isipokuwa kwa utapeli. Wafuasi wa papa wamekazana sana kuleta mashtaka ya uzushi dhidi ya Waprotestanti na dhidi ya kujitenga kwao kwa makusudi toka katika kanisa lao la kweli. Lakini mashtaka hayo ndiyo hasa yanayowahusu wao wenyewe. Wao ndio walioitupa chini bendera ya Kristo na kujitenga mbali na ile “imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.” Yuda 3.Mgunduzi wa Mafundisho ya Uongo Shetani alijua fika ya kwamba Maandiko yale Matakatifu yangewawezesha wanadamu kuyang’amua madanganyo yake na kuupinga uwezo wake. Ilikuwa ni kwa njia ya Neno hilo hata yule Mwokozi wa ulimwengu aliweza kuyapinga mashambulio yake. Kwa kila shambulio lake [Shetani], Kristo alionyesha ngao ya ile kweli ya milele, akisema, “Imeandikwa.” Kwa kila shauri alilotoa yule adui, alikataa kwa kutegemea hekima na uwezo wa lile neno. Ili huyo Shetani apate kudumisha utawala wake juu ya wanadamu, na kuimarisha mamlaka ya tapeli yule wa kipapa, ilikuwa ni lazima kwake kuwaweka watu katika hali ya ujinga wa kutoyajua Maandiko. Biblia ingemtukuza Mungu na kuwaweka wanadamu mahali pao panapowastahili hasa; kwa hiyo ilikuwa ni lazima kwamba zile kweli zake takatifu zifichwe kwa watu na kupigwa marufuku. Mantiki hiyo ikatumiwa na Kanisa la Roma. Kwa mamia ya miaka uenezaji wa Biblia ulipigwa marufuku. Watu walikatazwa kuisoma au kuwa nayo katika nyumba zao, na makasisi (mapadre) pamoja na maaskofu wapotovu wakayafafanua mafundisho yake ili yapate kuunga mkono unafiki wao. Hivyo ndivyo papa alivyokuja kutambulikana karibu ulimwenguni kote kama Kaimu wa [Aliye Badala ya] Mungu hapa duniani, ambaye alipewa mamlaka juu ya kanisa na serikaliKuelewa Unakokwenda Upapa, Angalia Historia Yake IliyopitaKuupigia Magoti Upagani Baada ya kuondolewa yule anayegundua mafundisho potofu [yaani, Biblia], Shetani akafanya kama apendavyo. Unabii ulikuwa umetangaza kwamba upapa unge“azimu kubadili majira na Sheria [Amri Kumi].” Danieli 7:25. Kazi hiyo [upapa] haukuchelewa kuanza kuifanya. Ili kuwapa waongofu waliotoka kwenye upagani kitu fulani badala ya ibada yao ya sanamu, na kukuzia upokeaji wao wa Ukristo kwa jina tu, kuabudu sanamu na mabaki ya mifupa ya watakatifu waliokufa zamani vikaingizwa taratibu katika ibada ya Kikristo. Amri iliyotolewa na baraza kuu hatimaye ikauimarisha mfumo huo wa ibada ya sanamu. Kuikamilisha kazi hiyo ya kukufuru, Roma ikadhamiria kuifutilia mbali kutoka katika Sheria ya Mungu [Amri Kumi] amri ile ya pili inayokataza ibada ya sanamu, na kuigawa amri ile ya kumi ili kuhifadhi idadi ile ile [ya Amri Kumi].

ConversionConversion EmoticonEmoticon