MFALME WA AMANI ANAKUJA UPESI SANA
(SOMA DANIELI 2 YOTE)
Mpendwa nnakukaribisha katika mfululizo wa masomo ya unabii kutoka katika kitabu cha Daniel ,kumbuka anaheri asomaye na wale wanaosikia neno la Mungu ,hivyo hautajuta kujifunza masomo haya Bwana akubariki unapofuatilia kupitia ukurasa huu .
Katika historia ya ulimwengu huu
Hakuna mwanadamu ye yote awezaye kutabiri kwa hakika mambo yatakayokuja baadaye kwa hekima au maarifa yake mwenyewe. Wanajimu [wanaobashiri kwa kuangalia nyota], wachawi wanaotazama bao, wasoma viganja, hata wana sayansi wanabahatisha tu, hawawezi kujua kwa hakika mambo ya zamani au mambo yanayokuja mbele hebu na tusome haya mafungu twende kwa wamoja (Dan.2:27,28; Isa. 42:8,9; 46:9,10; 41:21-24; 8:19; Yak. 4:13-16). Ni Mungu peke yake anayejua mambo ya zamani na yale yajayo, naye anatuambia kabla hayajatokea. Tangu dhambi iingie duniani mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu yalikatika; anawasiliana nasi kupitia kwa manabii anaowachagua mwenyewe (Isa.59:2; Hes. 12:6). Matukio yote makubwa yanayoleta maafa kwa wanadamu anawajulisha manabii wake (Amosi 3:7). Kuhusu Gharika alimjulisha Nuhu; kuangamizwa kwa Ninawi alimjulisha Yona; kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora alimjulisha Ibrahimu. Mbele yetu kuna mapigo saba hebu soma hilifungu(Ufunuo 16) ambayo yatawaathiri sana wanadamu. Kabla hayajaja alimjulisha Yohana kisiwani Patmo. Maafa yaliyotiishiwa yanaweza kuepukwa kama watu wanaohusika watatubu na kuacha dhambi zao (Yer. 18:7-10; Yona 3:1-10). Tukiwakataa manabii wanaotumwa na Mungu hatutafanikiwa katika safari yetu ya mbinguni (2 Nya. 20:20). Japo vitabu vya Biblia vilifungwa (Vitabu 66 - Agano la Kale 39; Agano Jipya 27), bado manabii wataendelea kutumwa na Mungu kulionya kanisa lake (Yoeli 2:28-31; Efe.4:11-14). Kwa kuwa wako manabii wa uongo, basi, yatupasa kuwapima. Viko vipimo vinne ambayo nabii ni lazima atimize vyote kuweza kukubalika kama nabii wa kweli wa Mungu -----
hebu soma haya mafungu
1. Yer. 28:9; Kum. 13:1-5;
2. Isa. 8:20 [Kut.20:3-17];
3. Mt. 7:20;
4. 1 Yoh. 4:1-3). Kupitia haya mafungu ndipo Unaweza kumtambua nabii wa kweli ,lakini asipoenda Sawa na neno hili huyo sio nabii wa kweli ,je, umeweza kutofautisha ?.
Kumbuka kuwa Unabii na Historia vinakwenda bega kwa bega (Yohana 14:29). Tafsiri sahihi ya unabii itaungwa mkono na mafungu ya Biblia na Historia (Isa. 28:10; 2 Pet. 1:19-21).
Unabii hautafsiriwi kama mtu apendavyo au kama kanisa fulani lipendavyo .
je , wewe ndoto unazichukuliaje ?
Ndoto aliyoota mfalme iliyomfadhaisha sana ilihusu Falme Kuu Nne zilizotawala dunia na Falme zilizofuata hadi kuja kwa Yesu Kristo kuja kusimamisha ufalme wake wa milele. Tafsiri ni hii:
I. UFALME WA BABELI
Ulitokea miaka ya(606-538 au 605-539 K.K.).
Umewakilishwa na
Kichwa cha dhahabu
(Dan. 2:37-38). Historia inaunga mkono.
II. UFALME WA WAMEDI NA WAAJEMI
Ulitokea kati ya mwaka (538-331 au 539-331 K.K.). Uliuangusha Ufalme wa Babeli (Dan. 5:25-31). Unawakilishwa na Kifua na Mikono ya Fedha (Dan. 2:32a,39a).
Historia inaunga mkono. Miaka ni ya kukadiria tu.
III. UFALME WA WAYUNANI
(331-168 K.K.)
Ufalme wa Wamedi na Waajemi ulitabiriwa kuwa utaangushwa na Wayunani (Dan. 8:4-7,20-21; 11:13).
Ufalme wa Wayunani (Wagiriki) unawakilishwa na Tumbo na Viuno vya Shaba (Dan. 2:32b,39b). Historia inaunga mkono.
IV. UFALME WA WARUMI (168 K.K. - 476 B.K.).
Ufalme wa Warumi unawakilishwa na Miguu ya Chuma. Biblia inaielezea vizuri Dola ya Warumi kuwa ilikuwa inazivunja-vunja falme zile nyingine kama chuma. Danieli hakujulishwa jina la Dola hii. Lakini historia inathibitisha kuwa Warumi waliwashinda Wayunani mwaka ule wa 168 K.K. Wakati Kristo anazaliwa Dola hiyo ilikuwa bado inatawala dunia pamoja na Palestina chini ya Kaisari Augusto (Luka 2:1-7; Yohana 11:48)
UFALME WA PAPA (538-1798 B.K.)
Ulitokea katika mabaki ya Dola ya Warumi baada ya kuangushwa na makabila ya [kipagani] ya Ulaya Kaskazini mwaka wa 476 B.K. Unawakilishwa na Nyayo za miguu (Dan.2:33b,41a). Udongo unawakilisha kanisa au watu wa Mungu (Isa.64:8; Yer. 18:6). Chuma kinawakilisha serikali. Hivyo kuchanganyika kwa udongo na chuma ni muungano wa dini na serikali chini ya kiongozi mmoja wa kidini wa Roma. Historia inathibitisha kwamba ufalme huu uliinuka katika mabaki ya Dola ya Warumi baada ya kuangushwa na kutawala dunia kuanzia 538 B.K. Huu ni Utawala wa Papa au Upapa.
VI. FALME KUMI ZA ULAYA MAGHARIBI (476-MAREJEO YA KRISTO)
Falme kumi za Ulaya Magharibi zinawakilishwa na Vidole Kumi Vya Nyayo (Dan. 2:42). Falme hizo ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi (Switzerland), Ureno, Hispania, Italia, Waheruli (Heruli)*, Wavandali (Vandals)*, na Waostrogothi (Ostrogoths)*. Falme tatu za mwisho huwezi kuziona katika ramani ya siku hizi. Habari zake zitatolewa katika somo la Danieli 7. Mataifa hayo 10 yalikuwa makoloni ya Warumi. Rumi ilipoanguka mwaka 476 yakawa yamejikomboa na kuwa huru. Baadaye yalipoipokea dini ya Katoliki kwa nguvu yakajikuta yametawaliwa na Papa aliyejiita Mfalme wa wafalme kuanzia mwaka 538 B.K.
VII. UFALME WA MILELE WA KRISTO (MAREJEO YAKE HADI MILELE) Ufalme huo unawakilishwa na Jiwe lililochongwa bila kazi ya mikono (Dan.2:34,35,44,45). Jiwe hilo ni Kristo (Luka 20:17,18; Mt. 21:42,44; Mdo. 4:10-12). Huyo ndiye Mfalme wa Amani anayekuja upesi sana (Isa. 9:6; Ufu.22:12). Atakapokuja atazivunjilia mbali falme zote za dunia (Ufu.11:15; 19:11-21). Kuna kitabu katika kanisa la waadventista wa Sabato kiitwacho Majibu kwa Mashaka Yako somo la miaka 1000 itakayoanza atakapokuja Kristo mara ya pili. Baada ya kupita miaka hiyo 1000 waovu watafufuliwa na kuangamizwa katika moto wa milele pamoja na Shetani na malaika zake na kuwa majivu, ndipo dunia hii iliyoharibiwa vibaya wakati wa kuja kwake mara ya pili [Yer. 4:23-27; Ufu. 6:14-17] itakapofanywa kuwa mpya pamoja na mbingu yake (Ufunuo Sura ya 20; Mal. 4:1-3; Eze. 28:14-19; Ufu. 21:1; Zaburi Sura ya 37). Ombi letu la dhati lingekuwa ni hili: "Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako" (Luka 23:42). Ahadi ile ile itatolewa kwetu kuanzia leo tunapomwomba ombi hilo kama kweli tumedhamiria kuishi kwa ajili yake hapa duniani, "Utakuwa pamoja nami peponi" (Luka 23:43). Ndugu yangu, kwa nini leo hii uipoteze nafasi hii ya thamani? Kata shauri sasa kumfanya Yesu awe Bwana na Mwokozi wako. Itumie vizuri nafasi ya leo kama yule jambazi pale msalabani. Acha kucheza na dhambi. Leo ndiyo siku ya wokovu wako (2 Kor. 6:2).
YESU atakapokuja ataiangamiza dhambi kamwe haitakuwa na nafasi tena je Unajua anakuja lini ? ,toa maisha yako kwake leo ,mahala popote ulipo tafta kanisa la waadventista wa Sabato ujiunge na watu wanaomngoja kristo kwa hamu kubwa pale atakapo kuja washangilie kumlaki kwenda mbinguni ,usiangalie nani anafanya nini wewe jitoe na Mungu hatakuacha ubarikiwe unapofanya maamuzi ya kupata uzima wa milele kutoka katika mauti ya milele .
Mm mwinjilisti fredrick sylvanus nnapenda kukukaribisha tena kwa masomo yanayoendelea daima ushindi wa dhambi inawezekana tukijikabidhi kwa YESU pekee maana ndiye pekee aliyeishinda dhambi .
Ubarikiwe

ConversionConversion EmoticonEmoticon