JE , UTASIMAMA ITAKAPOAMRIWA.

Ninakukaribisha tena rafiki Mpendwa katika muendelezo wa kitabu cha Daniel ,leo tutaangalia jinsi ambayo Mungu amekuwa akitembea na wake waaminifu katika kila kizazi ,usishangae huenda leo anatumia pia watu kusimamia taratibu zake alizotoa ,pengine anakusudia pia kukutumia wewe cha ajabu haukuwa umegundua ,ashukuriwe Mungu kwa kuupata ujumbe huu uwe tayari kuupokea na uruhusu Mungu ajivunie kukuweka kuwa hai leo ,Karibu kwa somo
 (SOMA  DANIELI  3  YOTE)
Unaweza ukajiuliza maswali nini kilisababisha shetani kutupwa kutoka mbinguni hadi duniani , kumbuka kwamba
tangu mbinguni Shetani amekuwa akiipiga vita  Sheria  ya  Mungu  (Amri  Kumi). Anamkasirikia vibaya  sana kila mtu  anayezishika Amri  zote Kumi za Mungu  na Imani ya Yesu (Ufu.12:17;   14:12;   Kut. 20:3-17).   Mtu akishika  Amri tisa  katika hizo  kumi ni sawa na mtu ambaye hashiki hata moja;  Shetani hana shida na mtu  kama  huyo,  maana  yuko upande  wake;  hawezi  kumpiga  vita  hata  kidogo  (Yak.2:10-12).    Amri  Kumi  ndizo zinazoonyesha  dhambi,  kwa  maana  "Dhambi  ni  uvunjaji  wa  Sheria  [Amri  Kumi]"  (1 Yohana  3:4,  AJKK;   Rum.  7:7).   Inachukua  uvunjaji  wa  amri  moja  tu  kuwa  mwenye dhambi.   Kwa  hiyo,   Mkristo  ye  yote,  haidhuru  awe  nani  au  awe  na  cheo  gani, anayeidharau  Sheria  ya  Mungu  iliyotolewa  mlimani  Sinai (Amri  Kumi) yuko katika  hatari kubwa  ya  kupoteza  uzima  wa  milele  (1  Yoh.  2:3-6;  5:1-5;   Zab.  119:155).    Yesu  aliye kielelezo chetu na ambaye ni Mungu alishika Amri Kumi za Baba yake;  nasi kama wafuasi wake yatupasa kufuata kama yeye alivyoenenda(yohana15:10).   Usikubali  mtu  ye  yote  akudanganye, maana  "watu  wabaya  na  wadanganyaji wataendelea,  na kuzidi kuwa  waovu, wakidanganya na kudanganyika"  (2 Tim.3:13).  Hao waepuke.   Angalia  usijidanganye  mwenyewe  (Gal.  6:7,8),  wala  usimruhusu  kipofu akuongoze kipofu mwenzake,  mtatumbukia wote wawili shimoni (Mt.  15:14).  Uzima wa milele una thamani kubwa  kiasi  kwamba  mtu  hawezi  kukubali  kuupoteza  vivi  hivi  (Mt. 22:29). Hapa  tunawakuta  vijana  watatu  wa  Kiebrania  kasoro  Danieli  hayupo  safari  hii. Katika Danieli 1 tuliona jinsi vijana  wale  wanne  walivyoshinda  mtihani  ule  wa  chakula. Kula chakula au  kunywa kinywaji  kinachodhuru  mwili kwa  makusudi mazima  ni kuvunja Amri ya Sita  inayosema,  Usiue(Kut.20:13).
Hivyo  walishinda  mtihani wa Amri  ya Sita.  Sasa wamekabiliwa na mtihani mgumu kabisa wa Amri ya Pili  inayosema,    "Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa  kitu  cho  chote  kilicho  juu  mbinguni,  wala  kilicho chini  duniani,  wala  kilicho  majini  chini  ya  dunia.    Usivisujudie  wala  kuvitumikia..." (Kutoka 20:4-6).   Mfalme  Nebukadreza  baada  ya kuelezwa  maana  ya  ndoto  yake  aliyoota ya  sanamu  kubwa  katika Danieli  2  kuhusu  Falme zile  Kuu  Nne  ukiwamo na  ufalme wake akafanya  shingo  ngumu kupingana na Mungu.  
Akatengeneza sanamu kubwa  ya  dhahabu tupu  [dhahabu  iliwakilisha  ufalme  wa  Babeli]  akimaanisha  kwamba  ufalme  wa  Babeli utadumu milele.  Akataka sanamu hiyo iliyowekwa  katika uwanda wa Dura isujudiwe na wote  waliokuwapo  pale  (Dan.3:1-7).  
Wote  wakaisujudia  kasoro  wale  vijana  watatu Waebrania  -----  Shadraka, Meshaki,  na  Abednego.    Ni  ujasiri  ulioje  katika  halaiki  ile walimokuwamo viongozi wakuu  wa  serikali ya  Babeli!   Watu  wa  Mungu  wanatakiwa kuwa na ujasiri  kama  huo  kutetea  kweli ya  Mungu  hata  kama mbingu  zinadondoka  
(Rum.  8:3539;  Ebr. 11:32-40;  Dan. 11:33).
 Mfalme  alijaribu  kuwasihi  wafanye  hivyo  mara  watakaposikia tena filimbi  na  ngoma zikipigwa.  Akawatishia kuwa  atawatupa  katika  tanuru  ya  moto  iliyokuwa kali mara saba kuliko kawaida.  Lakini wao kwa upole wakasema,  "Mfalme,    Ee  Nebukadreza,  hamna haja  kujibu  katika  neno  hili.   Kama  ni  hivyo,    Mungu  wetu  tunayemtumikia  aweza kutuokoa  na  tanuru  ile  iwakayo  moto;    naye  atatuokoa  na  mkono  wako,    Ee  mfalme.   Bali kama  si hivyo, ujue,   Ee  mfalme,  ya  kuwa  sisi  hatukubali kuitumikia miungu  yako, wala kuisujudia  hiyo  sanamu  ya  dhahabu  uliyoisimamisha"   (Dan.  3:16-18).   Ndipo  mfalme akakasirika  sana  na  kuamuru  wafungwe  na  kutupwa  na  wanajeshi  mashujaa  ndani  ya tanuru  ile  ya  moto.   Wale  waliowatupa  walikufa  kwa  ukali  wa  moto  ule.    Hatimaye wakafanikiwa kuwatupa katikati ya ile tanuru iliyowaka moto.  Je! kulitokea nini?Loo!   mfalme  akashangaa, hatukutupa watu  watatu,  mbona  wako  wanne,  na  mmoja anakuwa  kama  mwana  wa  miungu  [Yesu  alikuwa  pale  kuwaokoa].   Ameahidi  kuwa atakuwa  pamoja  na  watu  wake  mpaka  mwisho  wa  dahari  (Mt.  28:20).    Hata  wakipita motoni  au katika  maji  mengi  atakuwa  pale tayari kuwaokoa  (Isaya  43:1,2).   Alitimiza ahadi yake  kwao  katika tukio  lile la  kutisha.   Wakawa  wanatembea  ndani ya  moto bila  kuungua. Walipotolewa nje ya tanuru ile "wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu  juu  ya  miili  yao,  wala  nywele  za  vichwa  vyao  hazikuteketea,  wala  suruali  zao hazikubadilika,  wala  harufu  ya  moto  haikuwapata  hata  kidogo"  (Dan.  3:27).    Bwana asifiwe!!!   Ana  uweza  wa  kuokoa  kabisa!   Mungu  anasema,    "kwa  maana  wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa  kuwa  si  kitu" (1 Sam. 2:30).  Ndugu yangu, je! utasimama imara kutetea Amri Kumi za Mungu? Mfalme akatambua kuwa "hakuna Mungu mwingine awezaye  kuokoa  namna  hii. Kisha  akawakuza  [akawapandisha  cheo]  Shadraka,  na  Meshaki,  na  Abednego,  katika wilaya ya Babeli"   (Dan.  3:29,30);    akawadharau  wale  wote  walioisujudu  sanamu  ile  na kutoa amri kuwa wakisema neno lo  lote juu ya Mungu  wa vijana hao watakatwa  vipande vipande  na  nyumba  zao  zitafanywa  jaa  [la  takataka].    Hiyo  si  dharau  kubwa?    Kuna thawabu  katika  kusimama  imara  kutetea  kweli  ya  Mungu.   Yusufu  alifungwa gerezani  kwa kukataa  kuzini,  yaani, kuvunja Amri  ya  Saba (Kut. 20:14).    Matokeo  yake  Mungu  alikuwa naye gerezani  na hatimaye  alitolewa  na kuheshimiwa  kwa  kupewa  cheo  cha  Waziri Mkuu wa  Misri  (Mwa.39:21-23;  41:37-44).   Babeli  inawakilisha  nguvu  za  giza  [Shetani] zinazopigana na Amri Kumi za Mungu.  Hata Babeli  Mkuu  wa  Ufunuo  anayo  tabia  iyo hiyo.   Shetani  anaitumia  Babeli  kutekeleza maangamizi yake  juu ya  watu  wa  Mungu  wasio na hatia. Kizazi hiki cha mwisho cha  Sayansi na Teknolojia kitakabiliwa  na Mtihani Mgumu kuliko  yote  wa  Amri  ya  Nne  ihusuyo Sabato  (Kut.  20:8-11).  Yohana alionyeshwa kwamba kila mtu aliye hai wakati huo  atajaribiwa  (Ufu.  3:10).    Watakaolindwa  na  Kristo  ni  wale waliolishika  neno la  subira yake  (Ufu.14:12)  ----   "Hapa ndipo  penye  subira  ya watakatifu, hao  wazishikao  Amri  [Kumi]  za  Mungu  na  Imani  ya  Yesu".  
 Je!  utasimama  chini  ya Bendera ya Imanueli iliyoandikwa  maneno hayo juu [Ufu. 14:12]  au chini ya Bendera ya Chapa ya Mnyama [Ufu. 13:16,17]   -----  iliyoandikwa  siku  ya kupumzika ya  kizazi kipya kijacho?  
Hebu kwa neema yake  Mungu na tuazimie kwamba 'hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli,  bali kwa ajili ya kweli"  (2 Kor. 13:8).  Lakini  kweli ni nini? Neno la Mungu ni kweli;  Sheria ya  Mungu (Amri Kumi) ni kweli  (Yoh. 17:17;  Zab. 119:142).
 Neno  lake  na  Sheria  yake  hudumu  milele  (Mt.  25:35;    1  Pet.  1:23;    Luka  16:17;    Zab. 119:44).  
Sheria yake ni "kamilifu";  hivyo  huwezi kuongeza wala kupunguza kitu katika Sheria hiyo ya Amri Kumi (Zab. 19:7;  Kum. 4:2,10-13).

Ndugu Mpendwa kama tulivyoona kwa kupitia somo ,muda sio mrefu ufalme wa rumi utasimama tena na kuamuru wanadamu wote kuisujudia alama ya mnyama manayeke ni kukubali kuabudu siku ya kwanza ya Juma (jumapili) .badala ya Juma mosi ,nikama vile wale vijana waebrania wakati wakiwa babeli walikuwa wamefundishwa kumtumikia Mungu na kumcha pekee bila kukengeushwa na mafundisho mengine kama yalivyo leo ,ndugu nnakuomba ukubali kujifunza neno la Mungu kwa kuzifahamu hasa vyema amri zake kumi (KUTOKA 20:3-17.)huwezi kuelewa kwa urahisi uhusiano uliopo kati ya amri kumi na wokovu ,Karibu kwa kanisa linalofundisha amri zote kumi kanisa la waadventista wa Sabato popote ulipo waweza kulipata kama utakuwa na swali juu ya masomo haya tahadhali usisite kuuliza
.

Ninakukaribisha kwa somo linalofuata ambalo nimhimu sana kwa hatima ya maisha YETU .Bwana akubariki sana .




Previous
Next Post »