MFALME WA KASKAZINI KUHAMIA YERUSALEMU
(SOMA DANIELI 11 YOTE)
Karibu Mpendwa tunapoendelea na unabii wa biblia kutoka katika kitabu cha Daniel ,kumbuka kuwa katika kila utawala au ufalme Mungu ndiye anayeruhusu hawa watawala kuongoza lakini pia Mungu hawasahau wafalme wanaofanya mapenzi yake na kuwasaidia watu wake wanapopigwa vita na Shetani akitumia wanadamu kuwashtaki. Wanadamu wanapotaka kuivuruga au kuikomesha kazi ya Mungu, ujue nyuma yake yuko Shetani; anawatumia.
Vita vikubwa [Pambano Kuu] vinaendelea nyuma ya pazia. Hatuwezi kuviona kwa macho yetu. Koreshi, Mwajemi, ndiye aliyeyaongoza majeshi yaliyoiangusha Babeli usiku ule wa mwisho kwa Belshaza (Dan. 5:25-31). Alimwachia utawala wa Babeli mjomba wake Dario, Mmedi. Kama bado unakumbuka masomo yaliyopita, Dario alimpenda sana Danieli na kumpa cheo cha Waziri Mkuu. Pia alimpenda sana Mungu wa Danieli. Kwa hiyo malaika Gabrieli alitumwa kumthibitisha katika kiti chake cha enzi na kumtia nguvu (Dan. 11:1). Alipotawala Babeli alikuwa mzee wa miaka 62; baada ya kufa kwake Koreshi alitawala Babeli (Dan. 10:1).
Katika Danieli 11 tunaziangalia falme zile zile kuanzia Ufalme wa Wamedi na Waajemi mpaka hapo Ufalme wa Kristo utakaposimamishwa. "Kusimama" maana yake kutawala. Ufalme wa Babeli ulikuwa umeangushwa tayari na Wamedi na Waajemi. Sura hii imeandikwa kwa lugha ya kawaida inayoeleweka vizuri kwa kila mtu.
Kwa hiyo haitakuwa na shida sana katika kuuelewa , Unabii huu unaendelea kutoka Sura ile ya 10; Gabrieli anazidi kumweleza Danieli mambo yatakayowapata watu wa Mungu katika siku za mwisho (Dan. 10:1). Ajabu ni kwamba sehemu kubwa sana ya unabii huu tayari imekwisha timia. Wahusika katika pambano hili wameelezwa wazi kwa kuonyesha vitendo vyao ambavyo vilitimia mia kwa mia. Jukumu letu hapa ni kuwataja kwa majina yao wahusika muhimu wachache kutoka katika historia ambao walitimiza mafungu yaliyoonyeshwa katika mibano mbele ya majina yao. Hebu sasa na tuwapitie mmoja baada ya mwingine. Wahusika wakuu katika Ufalme wa Wamedi na Waajemi:
Dario (Dan. 11:1); Koreshi (Dan. 10:1); wafalme watatu wa kwanza waliofuatana (Dan. 11:2) ambao ni Kambises, mwanawe Koreshi; Smerdisi; na Dario Histaspes. Yule wa nne aliyekuwa tajiri kuliko wote ni Ahasuero, huyo ndiye aliyechokoza vita juu ya ufalme mdogo wa Uyunani ambao baadaye uliuangusha Ufalme wa Wamedi na Waajemi.
Wahusika wakuu katika Ufalme wa Wayunani: Iskanda Mkuu (Alexander the Great) (Dan.11:3,4) ----- alipokufa akingali kijana mbichi hakuacha uzao (mtoto) wa kumrithi.
Kwa hiyo majenerali wake wanne wakagawana ufalme wake katika majimbo manne (Dan. 11:4);
majina yao ni haya:
Cassander, Lysimachus, Seleucus, na Ptolemy. Katika ukoo wa Seleucus walitawala wafalme wengi zaidi ya 20 kabla ya Ufalme wa Wayunani kuangushwa na Warumi. Mmojawapo ambaye hakuwa mashuhuri kama baba yake ni yule Antioko Epifani (Antiochus Epiphanes IV) ambaye watu wengine wanamdhania kuwa ndiye "Pembe Ndogo" ya Danieli 7 na 8. Pamoja na kwamba aliwatesa Wayahudi kwa miaka 3 na siku 10 na kulinajisi Hekalu lao, hatimizi vigezo vyote vya "Pembe Ndogo". Alikufa vitani mwaka 164 K.K. ambapo "Pembe Ndogo" ya Danieli 8 itaondolewa madarakani na Mungu mwenyewe (Dan. 8:25); wala hakupambana na Kristo ana kwa ana kwa vile alikufa kabla ya kuzaliwa Kristo, wala hawezi kuwa tishio kwa ulimwengu katika siku hizi za mwisho kama ilivyo hiyo "Pembe Ndogo" ya Danieli 7 na 8. Majenerali hao wanne wa Kiyunani waliendelea kupigana wao kwa wao hadi mwisho; Seleucus akachukua eneo lote la Mashariki (makao makuu yakiwa Siria), Kaskazini, na Magharibi Ulaya. Ptolemy akaendelea kubaki na eneo la Kusini (Misri).Kijiografia wafalme hao wawili waliobaki wakaitwa "Mfalme wa Kaskazini" (Seleucus) akikaa Siria, na "Mfalme wa Kusini" (Ptolemy) akikaa Misri.
Ukoo wa kila mfalme uliendelea kutawala hadi Warumi walipoingilia kati. Wahusika wakuu katika Falme hizo mbili za Kiyunani ni hawa: Ptolemy Philadelphus ----- mfalme wa kusini (Dan. 11:6), binti yake ni Bernice, aliyekwenda kuolewa kwa Antiochus Theus, mfalme wa kaskazini aliyekuwa na mke wake wa kwanza Laodice (Dan. 11:6). Laodice akijaa wivu alimwua kwa sumu Bernice, na mtoto wake mchanga aliyemzaa, pamoja na wajakazi wake, na mumewe. Kaka yake Bernice aliyeitwa Ptolemy Eurgetes, chipukizi la mizizi yake, alikwenda kulipiza kisasi cha kuuawa dada yake kwa mfalme wa kaskazini (Dan. 11:7-13). Hatimaye Warumi wakaingia katika mandhari hiyo ya vita za kulipizana kisasi kwa wafalme hao wa Kiyunani. Wahusika wakuu katika Ufalme wa Warumi:
Ufalme wa Warumi unaingia katika fungu la 14 hadi la 16 la Sura hii. Cleopatra, binti wa watu [wa mfalme wa Misri], alipelekwa kwa Kaisari Julius (Julius Caesar) kama zawadi ya uzinzi ili ampendelee katika ugomvi wa utawala na kaka yake (Dan. 11:17-19); Kaisari Augusto, mpenda ushuru kwa anasa zake (Dan. 11:20; Luka 2:1-6). "Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba watu wote wa ulimwengu watozwe ushuru" (Luka 2:1, Tafsiri ya KJV). Yesu, Mkuu wa Maagano, aliishi na kuuawa chini ya Kaisari Tiberio (Dan. 11:21,22; Luka 3:1; Yoh. 18:15 - Kaisari Tiberio). Warumi waliingia Palestina na kuwaua Wayahudi (Dan. 11:23-29). Kusimamishwa kwa Chukizo la Uharibifu ni mwanzo wa Ufalme wa Papa au Upapa (Dan. 11:31-39) katika kipindi kile cha miaka 1260 cha Zama za Giza. Mauaji aliyofanya kwa watakatifu zaidi ya milioni 50 yameelezwa katika mafungu 32 na 33.
Matengenezo ya Kanisa (Reformation) yaliyoanzishwa mwaka 15l7 na Martin Luther na kufuatiwa na Wana-matengenezo wengine yaliwapatia maeneo ya kukimbilia waliokuwa wanateswa na kuuawa na Papa (Dan. 11:34; Ufu. 12:16; Mt. 24:15,21,22). Kwa njia hiyo mateso na mauaji yali"fupizwa" Mt. 24:22). Katika nchi za Kikatoliki yaliendelea hadi 1798. Ufalme wa Kirumi wa Kisiasa ulioangushwa unaendelezwa mpaka leo chini ya Upapa.
Mfalme wa Kaskazini wa Siku za Mwisho Kuhamia Yerusalemu: Mfalme huyo ni tofauti na wafalme wale wa Kiyunani walioitwa "Mfalme wa Kaskazini" na "Mfalme wa Kusini" kuanzia fungu la 5 hadi la 17. Ametajwa katika fungu la 40 hadi 45. Mambo yanayomhusu "Mfalme wa Kusini" wa siku za mwisho katika mafungu hayo bado hayajabainishwa. Dhana zipo nyingi. Yesu alisema, "Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini" (Yoh. 14:29). Unabii unaposema kusini ni kusini kwa mfalme huyo wa kaskazini; nchi zitakazopinduliwa zimetajwa pamoja na nchi zitakazompatia hazina. Mfalme wa Kaskazini wa siku za mwisho ni Ufalme wa Papa au Upapa utakapotawala katika awamu yake ya pili na ya mwisho (Dan. 11:45; Ufu. 17:811). Ufalme huo unakwenda kuangamizwa vibaya na Mikaeli [Kristo] hapo atakaposimama [atakapotawazwa mbinguni katika sherehe iitwayo Arusi ya MwanaKondoo, atakabidhiwa Jiji Yerusalemu Mpya tayari kumkaribisha mkewe (kanisa) atakapomnyakua toka duniani wakati wa kuja kwake mara ya pili] (Dan. 12:1; Ufu. 19:6-9; 21:9,10). Kwa hiyo, Papa atakapohamia Yerusalemu, "naye ataweka hema zake za kifalme [makao makuu] kati ya bahari [ya Kati] na Mlima Mtakatifu [Mlima wa Mizeituni] wa uzuri [Palestina]" atakuwa anautimiza unabii huu. Lakini akiwa pale "ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia" (Dan. 11:45), "naye aenenda kwenye uharibifu" (Ufu. 17:11). Ni ajali gani atayopata, ni uharibifu [maangamizi] gani atapata? Soma Ufu. 19:11-21).ni hakika mnyama ataangamizwa kabisa na wale wote watakao ambatana naye wote wataangamizwa ,jina la Bwana litukuzwe maana hutupatia kila jambo tahadhali yake kabla halijatokea hivyo haya mambo ni hakika na kweli yanatokea wakati unaotujia ,hasa pale itakapotangazwa alama ya mnyama ndipo utengano utakapoonekana kati ya wale wanaoipokea na wale wasioipokea wito wangu kwako rafiki ni kwamba jifunze zaidi juu ya huu unabii na ule wa ufunuo, lakini usiogope maana kuna kundi kubwa la waaminio wale ambao hawatakubali kuipokea hiyo hapa ya mnyama nao hao watu watajazwa NGUVU na Mungu mwenyewe kwaajili ya kusimamia kweli yake ,kwahiyo kama ambavyo Mungu amekuwa akitembea na mashahidi wake kwa kila zama hata leo kuna watu watakaokuwa tayari kuuawa kwa kusimamia kweli ya Mungu, je wataka kuwafahamu wako hapa (ufunuo 14:12) nao watamshinda huyo joka kwa damu tu ile ya mwanakondoo ,ninapenda kukukaribisha katika kundi kubwa hili linaloipeperusha bendera ya YESU bila kupindisha ukweli ,lakini kumbuka kuwa hawa watu kwa namna flani hubezwa sana na kudharauliwa lakini ndivyo wanavyoenenda hata YESU atakapokuja watamlaki wakisema huyu ndiye tuliyemngoja kwa muda mrefu atuchukue ,Karibu katika hili kundi Mpendwa tunapoendelea katika kujifunza neno Kwa maandalizi ya utimirifu wa unabii nakisha tumngoje YESU ajapo kwa Mara ya pili.

ConversionConversion EmoticonEmoticon