SHERIA YA MUNGU
-I Usiwe na miungu mingine ila mimi.
-II Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu Mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudu wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu Wanipendao, na kuzishika amri zangu.
III Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
- IV Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; Lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya Mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; Kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. -V Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
VI Usiue.
VII Usizini.
VIII Usiibe.
IX Usimshuhudie jirani yako uongo.
X Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako, mtumwa wake, wala mjakazi , wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako. Kutoka 20:3-17
SHERIA YA MUNGU KAMA ILIVYOBADILISHWA NA MWANADAMU -
-I Mimi ni Bwana Mungu wako, Usiwe na miungu migeni ila mimi. (Amri ya Pili Imeachwa.)
-II (Hii hasa ni ya III) Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako.
III (Hii hasa ni ya IV) Kumbuka kwamba unaitakasa siku ya Sabato. (Amri ya Sabato imebadilishwa vibaya sana!)
IV (Hii hasa ni ya V) Waheshimu baba na mama yako.
V (Hii hasa ni ya VI) Usiue.
VI (Hii hasa ni ya VIIUsizini.
VII (Hii hasa ni ya VIII) Usiibe.
VIII (Hii hasa ni ya IX) Usimshuhudie jirani yako uongo.
IX (Hii hasa ni ya X, Sehemu ya Kwanza) Usimtamani mke wa jirani yako.
X (Hii hasa ni ya X, Sehemu ya Pili) Usitamani mali ya jirani yako.
Katekisimu ya Wote ya Kikatoliki
.Maridhiano Yaendelea .
Roho ile ya maridhiano na upagani ikafungua njia ya kutoijali sana Mamlaka ile ya Mbinguni.
Shetani, akifanya kazi yake kwa kuwatumia viongozi wa kanisa wasiojitoa wakf kwa Mungu, akaigeuza amri ile ya nne pia, na kujaribu kuiweka kando Sabato ile ya kale [Jumamosi], siku ambayo Mungu alikuwa ameibarikia na kuitakasa, na mahali pake kuitukuza sikukuu iliyoadhimishwa na makafiri kama “siku tukufu ya jua” [Jumapili]. Badiliko hilo mwanzoni halikufanywa waziwazi.
Katika karne zile za mwanzo Sabato ya kweli [Jumamosi] ilikuwa imetunzwa na Wakristo wote. Walikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu, na, wao wakiwa wanaamini kwamba Sheria ya Mungu [Amri Kumi] haibadiliki kamwe, basi, kwa bidii nyingi walitunza utakatifu wa amri zake [kumi]. Lakini kwa usiri mkubwa Shetani alifanya kazi yake kupitia kwa vibaraka wake ili kutekeleza lengo lake. Ili mawazo ya watu yapate kugeuzwa kuelekea kwenye ile Jumapili, ikafanywa kuwa sikukuu ya kuheshimu ufufuo wa Kristo.
Ibada za dini zikaigeukia siku hiyo; lakini bado ilifikiriwa kama siku ya mapumziko tu, Sabato [Jumamosi] ikiwa inaendelea kutakaswa. Kutayarisha njia kwa ajili ya kazi ile aliyokusudia kuifanya, Shetani akawaongoza Wayahudi, kabla ya kuja kwa Kristo, kuiwekea Sabato mizigo mizito na masharti makali, wakifanya utunzaji wake kuwa mzigo mzito ulemeao. Basi, [Shetani] akiitumia nafasi hiyo ya kuwapo kwa nuru ile ya uongo ambayo kwayo aliifanya [Sabato] ifikiriwe vibaya, akaifanya ipate kudharauliwa na watu kama siku ya wayahudi. Wakati Wakristo wakiendelea kwa kawaida kuiadhimisha Jumapili kama sikukuu ya furaha, akawaongoza kuifanya siku ya Sabato [Jumamosi] kuwa siku ya kufunga [saumu], yaani, siku ya huzuni na majonzi, ili kuonyesha chuki yao dhidi ya dini ile ya Kiyahudi.
Badiliko la Kijasiri
Katika sehemu ile ya kwanza ya karne ya nne mfalme Konstantino alitoa amri na kuifanya Jumapili kuwa sikukuu ya serikali katika dola yote ya Waroma.
Siku hiyo ya jua [Jumapili] iliheshimiwa na raia zake wapagani, tena iliheshimiwa na Wakristo; ilikuwa ni sera ya mfalme yule kuunganisha mambo yale waliyoyapenda makafiri na Wakristo ambayo yalikuwa yanaleta mgongano. Alishurutishwa kufanya hivyo na maaskofu wa kanisa, wakiwa wamechochewa na tamaa ya ukuu na kiu ya mamlaka walitambua kwamba kama siku ile ile moja ingeadhimishwa na Wakristo na makafiri, basi, ingeweza kusaidia kupokelewa kwa Ukristo na wapagani wale na kwa njia hiyo kuendeleza mbele mamlaka na utukufu wa kanisa. Lakini Wakristo wengi wacha Mungu waliposhawishiwa polepole kuifikiria Jumapili kama ina kiwango fulani cha utakatifu, bado waliendelea kuitunza Sabato ya kweli [Jumamosi] kama takatifu kwa Bwana, tena waliitunza kwa kutii amri ile ya nne [Kut. 20:8-11]. Laghai yule mkuu [Shetani] alikuwa bado hajaikamilisha kazi yake. Akaazimu kuukusanya pamoja Ulimwengu wote wa Kikristo chini ya bendera yake na kutumia uwezo wake kupitia kwa kaimu wake, yaani, yule papa, mwenye majivuno mengi, aliyejidai kwamba alikuwa ndiye mwakilishi wake Kristo. Kupitia kwa wapagani wale walioongoka nusu-nusu, na kwa maaskofu wale wenye kutaka makuu, na kwa watu wa kanisa walioipenda dunia akalitimiza kusudi lake.
Mabaraza makubwa sana yakafanywa toka wakati hata wakati, na katika hayo viongozi wakuu wa kanisa walikutana kutoka pande zote zaulimwengu. Karibu katika kila baraza lililokaa, Sabato [Jumamosi] ambayo Mungu alikuwa ameianzisha ikasukumiwa chini kidogo zaidi, wakati ule ule Jumapili ikawa inainuliwa juu.
Hivyo ndivyo sikukuu ile ya kipagani [Jumapili] ilivyokuja kuheshimiwa hatimaye kama siku iliyowekwa na Mungu, na wakati ule ule Sabato ile ya Biblia [Jumamosi] ikatangazwa kuwa ilikuwa ni mabaki ya dini ile ya Kiyahudi, na watunzaji wake wakatangazwa kuwa wamelaaniwa.
Jumapili imewekwa na Wakatoliki, na madai ya kutaka itunzwe yanaweza tu kutetewa kwa kufuata kanuni za Kikatoliki….Toka mwanzo hadi mwisho wa Maandiko Matakatifu hakuna kifungu hata kimoja kinachotoa kibali cha kuhamisha ibada ya kila juma kutoka katika siku ile ya mwisho wa juma kwenda ile ya kwanza." Catholic Press, Sydney, Australia, Agosti, 1900.
Muhuri wa Muumbaji Waondolewa
Mwasi huyo mkuu alikuwa amefanikiwa kujiinua mwenyewe “juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.” 2 Wathesalonike 2:4. Akadiriki kuibadili amri ile ya pekee katika Sheria ya Mungu [Amri Kumi] ambayo bila kukosea hata kidogo inawaelekeza wanadamu wote kwa Mungu wa kweli, aliye hai. Katika amri ile ya nne [Kut. 20:8-11] Mungu anadhihirishwa kama ndiye Muumbaji wa mbingu na nchi, na kwa sababu hiyo yeye anatofautishwa na miungu yote ya uongo.
Ilikuwa ni kwa ajili ya kumbukumbu ya kazi ile ya uumbaji, ndiyo maana siku ile ya saba [Jumamosi] ilitakaswa [ilitengwa kwa matumizi matakatifu] kama siku ya mapumziko kwa kila mwanadamu. Ilikusudiwa kumweka Mungu aliye hai daima kataika mawazo ya wanadamu kama chimbuko la uhai wao na lengo la kicho chao na ibada yao. Shetani anajitahidi sana iuwageuza watu waache kumtii Mungu, na kuacha kutoa utii wao kwa Sheria yake [Amri Kumi]; kwa hiyo, juhudi zake anazielekeza hasa dhidi ya amri ile [ya Sabato] inayomwonyesha Mungu kuwa ni Muumbaji. Waprotestanti siku hizi wanasisitiza kwamba ufufuo wake Kristo katika siku ile ya Jumapili ndio ulioifanya siku hiyo kuwa Sabato ya Kikristo. Lakini ushahidi wa Maandiko unakosekana. Hakuna heshima kama hiyo iliyotolewa kwa siku hiyo [ya Jumapili] na Kristo au na Mitume wake.Muhuri wa Muumbaji Waondolewa Mwasi huyo mkuu alikuwa amefanikiwa kujiinua mwenyewe “juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.” 2Wathesalonike 2:4.
Akadiriki kuibadili amri ile ya pekee katika Sheria ya Mungu [Amri Kumi] ambayo bila kukosea hata kidogo inawaelekeza wanadamu wote kwa Mungu wa kweli, aliye hai. Katika amri ile ya nne [Kut. 20:8-11]
Mungu anadhihirishwa kama ndiye Muumbaji wa mbingu na nchi, na kwa sababu hiyo yeye anatofautishwa na miungu yote ya uongo. Ilikuwa ni kwa ajili ya kumbukumbu ya kazi ile ya uumbaji, ndiyo maana siku ile ya saba [Jumamosi] ilitakaswa [ilitengwa kwa matumizi matakatifu] kama siku ya mapumziko kwa kila mwanadamu. Ilikusudiwa kumweka Mungu aliye hai daima kataika mawazo ya wanadamu kama chimbuko la uhai wao na lengo la kicho chao na ibada yao. Shetani anajitahidi sana iuwageuza watu waache kumtii Mungu, na kuacha kutoa utii wao kwa Sheria yake [Amri Kumi]; kwa hiyo, juhudi zake anazielekeza hasa dhidi ya amri ile [ya Sabato] inayomwonyesha Mungu kuwa ni Muumbaji. Waprotestanti siku hizi wanasisitiza kwamba ufufuo wake Kristo katika siku ile ya Jumapili ndio ulioifanya siku hiyo kuwa Sabato ya Kikristo.
Lakini ushahidi wa Maandiko unakosekana. Hakuna heshima kama hiyo iliyotolewa kwa siku hiyo [ya Jumapili] na Kristo au na Mitume wake.
Toka Roma ya Kipagani Kwenda Roma ya Kipapa Katika karne ile ya sita upapa ulikuwa umejiimarisha sana. Kiti chake cha enzi kilikuwa katika mji ule wa dola [Roma], na Askofu wa Roma [Papa] akatangazwa kuwa ndiye kichwa cha kanisa lote. Upagani ukaupa upapa nafasi yake [Dan. 8:12; 12:11]. Yule Joka [Ibilisi na Roma ya Kipagani Ufu. 12:9,3] alikuwa amempa mnyama [mfalme – Dan. 7:17] “nguvu zake na kiti chake cha enzi, na uwezo mwingi.” Ufunuo 13:2. Na sasa ikaanza ile miaka 1260 ya mateso [mauaji] ya papa yaliyokuwa yametabiriwa katika unabii wa Danieli na Ufunuo. Danieli 7:25; Ufunuo 13:5-7. Wakristo wakalazimishwa ama kuuacha msimamo wao mnyofu na kuzikubali sherehe za kipapa pamoja na ibada yake, ama kuchomwa moto juu ya kitita cha kuni, ama kukabiliwa na mtu yule akataye vichwa kwa shoka. Basi, maneno ya Yesu yakawa yametimizwa, aliyosema: “Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha [watawaua] baadhi yenu.
Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.” Luka 21:16,17. Mateso yakaanzishwa rasmi dhidi ya wale waliokuwa waaminifu kwa ukali sana kuliko wakati wo wote uliopita, na dunia hii ikawa ni uwanja mkubwa wa vita. Kwa mamia ya miaka Kanisa la Kristo likapata kimbilio lake katika maeneo ya upweke na ya siri. Nabii yule asema hivi: “Yule mwanamke [Kanisa la Kristo la Kweli] akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko kwa muda wa siku [miaka – Eze. 4:6] elfu na mia mbili na sitini.” Ufunuo 12:6.
Katika Karne Zile za Mwanzo Sabato ya Kweli Ilitunzwa na WaKijasiri
ote.
Mbarikiwe kwa kusoma maana umepata kujua jinsi mambo yalivyobadirishwa na sasa mpango mpya mwingine uko mbioni ondoa hofu Bwana ndiye msaada wako mpokee , mshike naye atakushika . karibu kwa somo linalofuata.

ConversionConversion EmoticonEmoticon