ONYO LA MWISHO WA DUNIA SEHEMU YA TANO

ZAMA ZA GIZA ZAANZA

 Kule  kujipatia  mamlaka  yake  lile  Kanisa  la  Roma  ndio mwanzo  wa  Zama  za  Giza.   Kadiri  uwezo  wake  ulivyozidi kuongezeka,  ndivyo  giza  [yaani,  ujinga  wa  kutoijua  Biblia, Sayansi  na  Teknolojia]  lilivyozidi  kuwa  nene.   Imani ikahamishwa  kutoka  kwa  Kristo,  aliye  msingi  wa  kweli,  kwenda kwa  papa  wa  Roma.   Badala  ya  kumtegemea  Mwana  wa  Mungu kwa  msamaha  wa  dhambi  na  wokovu  ule  wa  milele,  watu wakamtazama  papa,  na  makasisi  (mapadre)  na  maaskofu  ambao alikuwa  amewakabidhi  mamlaka.  

Wakafundishwa  ya  kwamba papa  alikuwa  ndiye  mpatanishi  wao  wa  kibinadamu  na  ya kwamba  hakuna  hata  mmoja  ambaye  angeweza  kumwendea Mungu  isipokuwa  kwa  kupitia  kwake,  na  kwa  ajili  hiyo  yeye alipaswa  kupewa  utii  bila  swali  lo  lote.   Kwenda  kinyume  na matakwa  yake  ilikuwa  ni  sababu  ya  kutosha  ya  kutolewa  adhabu kali  sana  juu  ya  miili  na  roho  za  wale  wahalifu.   Kwa  njia  hiyo, mawazo  ya  watu  yakageuziwa  mbali  na  Mungu  na  kuelekezwa kwa  wanadamu  wawezao  kukosa,  kupotoka,  na  wakatili,  naam, zaidi  sana,  kwa  yule  mkuu  wa  giza  mwenyewe  [Shetani], ambaye  alitumia  uwezo  wake  kupitia  kwa  watu  wale.   Dhambi ikafichwa  katika  vazi  la  utakatifu.  
Maandiko  yanapozuiwa kusomwa  na  watu,  na  mwanadamu  anapokuja  kujiona mwenyewe  kuwa  ni  mkubwa  kuliko  wote,  hapo  ndipo tunapohitaji  tu  kutazamia  kuona  hila,  udanganyifu,  na  uovu unaoishusha  hadhi  ya  mwanadamu.   Katika  kuzitukuza  sheria  za wanadamu  na  mapokeo  ukaonekana  ufisadi  ambao  hutokea daima  wakati  Sheria  ya  Mungu  [Amri  Kumi]  inapowekwa kandoSiku za Hatari Kubwa Kristo.  
Zile  zilikuwa  ni  siku  za  hatari  kubwa  kwa  Kanisa  lake Waaminifu  walioibeba  bendera  yake  walikuwa  ni wachache  kweli  kweli.  
 Ingawa  ile  kweli  haikuachwa  bila kuwapo  mashahidi,  hata  hivyo,  wakati  fulani  ilionekana  kana kwamba  mafundisho  yale  ya  uongo  na  ushirikina  yalikuwa yameenea  kote,  na  dini  ile  ya  kweli  ilionekana  kana  kwamba ingeweza  kufutiliwa  mbali  duniani  kote.   Injili  ikawa imesahauliwa,  lakini  mitindo  ya  dini  ikaongezeka,  na  watu wakawa  wamelemewa  na  mizigo  mizito  waliyotwishwa  yenye masharti makali. Wakafundishwa  sio  tu  kumtazama  papa  kama  ndiye mpatanishi  wao,  bali  kutegemea  matendo  yao  wenyewe  ili kuweza  kulipa  fidia  ya  dhambi  zao.   Safari  ndefu  za  taabu kwenda  kuzuru  patakatifu,  kutenda  matendo  ya  kitubio,  kuabudu mifupa  ya  watakatifu  waliokufa  zamani,  kujenga  makanisa, kujenga  makaburi  ya  watakatifu,  na  altare  [madhabahu],  kulipa fedha  nyingi  kwa  kanisa   -   mambo  hayo  pamoja  na  matendo mengine  yanayofanana  na  hayo  yaliamriwa  ili  kuituliza ghadhabu  ya  Mungu  au  kupata  upendeleo  wake,  kana  kwamba Mungu  alikuwa  kama  wanadamu,  kuweza  kukasirishwa  kwa mambo  madogo  sana  yasiyo  na  maana,  au  kutulizwa  kwa kupewa zawadi au kwa maungamo (kitubio)!

Giza  lile  likaonekana  kana  kwamba  lilikuwa likiongezeka  kuwa  nene  zaidi.   Ibada  ya  sanamu  ikawa  ni  jambola  kawaida  kwa  watu  wengi.   Mishumaa  ikawashwa  mbele  ya sanamu  zile  na  sala  zikatolewa  kwa  sanamu  zile.  

Desturi  zile  za kipuuzi  kabisa  na  za  kishirikina,  hata  akili  zao  zenyewe zikaonekana  kana  kwamba  zimepoteza  uwezo  wake  wa kujitawala.   Wakati  wale  makasisi  (mapadre)  na  maaskofu wenyewe  walikuwa  wanapenda  anasa,  uasherati,  na  ufisadi, iliweza  kutazamiwa  tu  kwamba,  watu  wale  waliowategemea kwa  uongozi  wao,  nao  wangeweza  kuzama  katika  ujinga  na uovu wao.
Papa yule Mwenye Majivuno Hatua  nyingine  katika  dhana  za  kipapa  ilichukuliwa katika  karne  ile  ya  kumi  na  moja  wakati  Papa  Gregori  wa  Saba alipotangaza  ukamilifu  wa  Kanisa  la  Roma.  
Miongoni  mwa mawazo  yake  aliyotoa  lilikuwapo  wazo  moja  lililosema  kwamba kanisa  lile  [la  Roma]  lilikuwa  halijapata  kukosea  kamwe kulingana  na  Maandiko.   Lakini  ushuhuda  wa  Maandiko  hayo haukuambaatana  na  lile  dai  lake.   Papa  yule  mwenye  majivuno mengi  alidai  pia  kwamba  anao  uwezo  wa  kuwaondoa  wafalme katika  kiti  chao  cha  enzi,  kisha  akatangaza  kwamba  hakuna hukumu  yo  yote  aliyoitoa  yeye  ambayo  ingeweza  kubatilishwa [kugeuzwa]  na  mtu  ye  yote,  ila  kwamba  yeye  ndiye  alikuwa  na haki ya kuyabatilisha [kuyageuza] maamuzi ya wengine wote. Ni  tofauti  kubwa  ya  kushangaza  mno  jinsi  gani  kati  ya kiburi  kile  kilichojaa  uonevu  cha  papa  yule  mwenye  majivuno mengi  ukilinganisha  na  upole  na  unyenyekevu  wa  moyo aliokuwa  nao  Kristo,  ambaye  anajiwakilisha  mwenyewe  kama mmoja  anayebisha  katika  mlango  wa  moyo  akiomba  kuingia ndani,  ili  apate  kuingia  humo  na  kuleta  msamaha  na  amani,  na ambaye  aliwafundisha  wanafunzi  wake,  akasema:   “Na  mtu  ye yote  anayetaka  kuwa  wa  kwanza  kwenu  na  awe  mtumwa  wenu.” Mathayo 20:27
Giza Lazidi Kuwa Nene Karne  zile  zilipozidi  kusonga  mbele  zilishuhudia ongezeko  la  daima  la  uongo  katika  mafundisho  ya  dini yaliyotolewa  kutoka  Roma.  
 Hata  kabla  ya  kuanzishwa  kwa upapa  mafundisho  ya  wanafalsafa  wale  makafiri  yalikuwa yamezingatiwa,  nayo  yalitoa  mvuto  wake  ndani  ya  kanisa.
 Wengi  waliodai  kwamba  wameongoka  walikuwa  bado wanazing'ang'ania  itikadi  za  falsafa  yao  ya  kipagani,  na  si kwamba  tu  waliendelea  kujifunza  falsafa  hiyo  wao  wenyewe, bali  waliwashurutisha  wengine  kuipokea  kama  njia  ya  kueneza mvuto  wao  miongoni  mwa  makafiri  wale.  
 Makosa  mazito yakaingizwa  kwa  njia  hiyo  katika  imani  ya  Kikristo. Lililojitokeza  sana  katika  hayo  ni  ile  imani  kwamba mwanadamu  ana  roho  isiyokufa,  na  ya  kwamba,  akifa  bado anaendelea  kuwa  na  fahamu  zake.   Fundisho  hilo  la  dini likaweka  msingi  ambao  juu  yake  Roma  ilianzisha  sala  kwa  ajili ya  watakatifu  waliokufa  na  ibada  ya  Bikira  Maria.   Kutokana  na fundisho  hilo  pia  ukazuka  uzushi  uliosema  kwamba  wale  ambao hatimaye  hawataweza  kutubu  wataendelea  kuteswa  motoni milele  hata  milele,  fundisho  ambalo  liliingizwa  katika  imani  ya kipapa.Ndipo  njia  ikawa  imetayarishwa  ya  kuingizwa  [kanisani] mavumbuzi  mengine  ya  kipagani  ambayo  Roma  iliyaita  kwa jina  la  'Toharani'  (purgatory),  nao  wakalitumia  fundisho  hilo kuwatisha  makundi  ya  watu  wale  waliokuwa  wajinga  na washirikina.   Kwa  uzushi  wao  huo,  wanathibitisha  kwamba  pako mahali  pa  mateso,  ambapo  roho  za  wale  wasiostahili  adhabu  ya milele  zinapaswa  kuadhibiwa  kwa  ajili  ya  dhambi  zao,  na  ya kwamba,  kutoka  hapo,  zinapowekwa  huru  mbali  na  uchafu wake, roho hizo huingizwa mbinguni.

Aksante kwa kufuatilia haya masomo hakika ndivyo ulivyo ukweli amua kuufahamu zaidi utakuweka huru kisha Fanya maamuzi ya kuufuata Mungu akubariki karibu kwa somo linalifuata. 
Previous
Next Post »