KUFUNGUA SIRI YA PATAKATIFU

Kufungua Siri Ya Patakatifu

Ninawaarika tena wapendwa tunapoendelea na kujifunza neno la Mungu ni matumanini yangu tumeendelea kufuatilia unabii wa Daniel mpaka tumefika mwisho wa kitabu chote ,kwa wageni wasipate taabu masomo yote ya kitabu cha Daniel yamo kwenye hii blog.kumbuka pia tumekuwa tukiendelea na kitabu cha ufunuo sura ile ya pili kwa hiyo baada ya hili somo tutaendelea na ufunuo.

Tangu hapo awali maandiko ndio umekuwa msingi mkuu hasa kwa kanisa la masalio hivyo Maandiko ambayo yamekuwa msingi na kiini cha imani ya watu wa marejeo (Waadventista) kuliko yote ni yale yasemayo,
 “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakasika”  Daniel 8:14.

Kumbuka kuwa wanamatengenezo hapo awali juu ya hili fungu ambapo walifikili kutakaswa patakatifu nikurudi kwa yesu kitu ambacho kilipelekea watu kuuza mali zao na kumsubili yesu ambapo hakutokea kama walivyotarajia kwahiyo usemi huu umekuwa ukijulikana sana miongoni mwa wale waliokuwa wakikutazamia kurudi kwake Bwana kuliko karibu.  
Lakini Bwana hakutokea kwani ni ?

Waumini walifahamu kuwa Neno la Mungu halina kasoro, ni lazima walivyoutafsiri unabii, ndiko kuna makosa.  

Lakini basi kosa lilikuwa wapi?

 Mungu amewaongoza watu wake katika mkusanyiko mkuu wa marejeo.  Na wala asingewaacha wamalizikie gizani, katika huzuni kuu na kushutumiwa kwa aibu;  kana kwamba ni wahuni tu wanaotangatanga.
  Ingawa wengi waliacha msimamo wao wa kuutafsiri unabii, na kukanusha imani ya wale walioambatana nao, lakini wengine hawakuikana imani ambayo inathibitishwa na  Maandiko na Roho wa Mungu.
 Ilikuwa wajibu wao kushikamana na ukweli walioupata. Walijifunza maandiko kwa bidii na kwa maombi ili wapate kugundua kosa lao.  
Kwa kuwa kwa upande wa kuhesabu miaka ya unabii hawakuona kosa lolote.
Waligeukia fundisho lihusulo patakatifu.
Wakagundua kwamba hakuna andiko lolote linalosema kuwa dunia hii ndiyo patakatifu, kama wengi wanavyoamini.  Bali waligundua maelezo tele kuhusu patakatifu, asili yake na mahali pake pamoja na huduma zake, kama isemavyo:

  “Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida zake za ibada, na patakatifu pake pa kidunia.  Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya wonyesho ndipo palipoitwa patakatifu.  Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo patakatifu pa patakatifu yenye chetezo cha dhahabu sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fi mbo  ya  Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; na juu yake Makerubi ya utukufu yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari ya vitu hivi kimoja kimoja”   Waebrania 9:1-5.

 Patakatifu palikuwa ni hema iliyojengwa na Musa, kwa agizo la Mungu kuwa mahali patakatifu pa kukaa Mungu.

 “Na wanifanyie patakatifu, ili nipate kukaa kati yao” Kutoka 25:8.  

Hivyo ndivyo Musa alivyoagizwa.  Patakatifu na patakatifu pa patakatifu, vyumba hivyo vilitengwa na pazia.  Na pazia kama hilo lilifunga mlango wa chumba cha kwanza. Patakatifu Pa Patakatifu Mno. Katika patakatifu palikuwamo kinara cha taa upande wa kusini pamoja na taa zake saba zikiwaka mchana na mba  ulifukizwa kila siku moshiukipaa pamoja na sala za Waisraeli, mbele za Mungu.
 Katika patakatifu mno lilikuwamo sanduku lililonakishiwa kwa dhahabu ambalo lilikuwa likitunza amri kumi za Mungu.

 Juu ya sanduku kulikuwa na kiti cha rehema kikikabiliwa na makerubi wawili walioumbwa kwa dhahabu.  Katika chumba hiki kuwako kwa Mungu kulionekana daima kati ya makerubi.  Baada ya Waebrania kukaa Kanani, hema takatifu ilibadilishwa na hekalu lilijengwa na Sulemani, ambayo ingawa ilikuwa jengo la kudumu na kubwa lilifanya kazi ile ile ilikuwa na mfano ule ule; mpaka ilipobomolewa siku za akina Daniel ….. mpaka maangamizo yake na Warumi katika mwaka 70 Ad.
 Hii ndiyo hema takatifu duniani ambayo tunasoma habari zake katika Biblia.  Hema takatifu ya agano la kale.  

Lakini je, agano jipya haina hema takatifu?

Hapa ndugu tuwe makini ili tuone YESU leo ni nani kwetu.

 Msomaji na mtafutaji ukweli ukifungua kitabu cha Waebrania utaona kuwa agano jipya, au agano la pili huzungumzwa katika maneno hayo yaliyosemwa hapo kwanza “hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida zake na ibada, na patakatifu pake pa kidunia”.  
Tukigeukia kusoma sura iliyopita twasoma,

Basi katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili, “Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu”  Waebrania 8:1-2.

Hapa ndipo inafunuliwa hema takatifu ya agano jipya.

 Hema takatifu ya agano la kwanza ilifanywa na Musa, hii ya sasa imefanywa na Bwana.

 Katika hema ya kwanza waliohudumu ni makuhani wa kidunia, katika hii ya pili, Kristo kuhani wetu Mkuu huhudumu akiwa upande wa mkono wa kuume wa Mungu.

 Hema moja ilikuwa duniani, na nyingine iko mbinguni.

Hema iliyojengwa na Musa ilijengwa kwa kielelezo kile kile cha ile ya mbinguni.  Bwana aliagiza akisema,

Sawasawa na hayo yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani na mfano wa vyombo vyako vyote, ndivyo nitakavyofanya”  “Nawe angalia  ya kwamba uvifanye  kama mfano ulioonyeshwa mlimani”  Hema  ya kwanza ilikuwa mfano wa wakati ule ambamo  ndani yake sadaka na kafara zilitolewa”  patakatifu pake, “mfano wa mambo ya mbinguni”.  Makuhani walihudumu.  “Kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbingu”.  Kristo hakuingia patakatifu palipotengenezwa kwa mikono ndio mfano wa patakatifu halisi, lakini aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu”  Kutoka 25:9-10.  Waebrania 9:23; 8:5; 9:24.
Hekalu la mbinguni ndilo asili ya hema lililojengwa na Musa ikiwa mfano.
  Uzuri wa hema la duniani ulionyesha mfano wa utukufu wa hekalu la mbinguni mahali ambapo Kristo anahudumu kwa ajili yetu mbele ya kiti cha enzi  cha Mungu.
 Ukweli wa hekalu la mbinguni na wokovu wa mwanadamu ulifundishwa hasa kwa huduma zilizofanyika katika hema takatifu la hapa duniani. Vyumba Viwili. Mahali patakatifu pa mbinguni palionyeshwa kwa njia ya vyumba viwili vya patakatifu pa duniani.  
Yohana alionyeshwa hekalu la Mungumiguu iliyochubuliwa huwaombea wanadamu walioanguka, ambao ukombozi wao umegharimu gharama ya jinsi hiyo.  “Na shauri la amani litakuwa kati yao wawili”  Upendo wa Baba ndio msingi wa ukombozi kwa wanadamu waliopotea.
 Yesu alisema kwa wanafunzi wake,  “Baba mwenyewe awapenda ninyi”  “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee …” Yohana 16:27; 2Kor. 5:19; Yoh. 3:16.
 
Siri ya Hema Takatifu Yadhihirika “Hema takatifu” ya kweli iliyoko mbinguni, ndiyo hema takatifu ya agano jipya.

 Kristo alipokufa huduma ambazo zilikuwa kivuli tu, zilikoma.

 Unadhani ni huduma gani hizi ? 

 Wakati Daniel 8:14 ilipotimizwa kama ilivyoamuriwa, patakatifu panapotajwa lazima pawe pale pahusupo agano jipya.
 
Hivyo basi unabi unaposema “hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa”  huzungumzia patakatifu pa mbinguni.

 Lakini kutakaswa kwa patakatifu humaanisha nini?

  Je, inawezekana kuwa ni kitu mbinguni kinachohitajika kutakaswa?

 Katika Waebrania 9 utakaso wa patakatifu na duniani na pa mbinguni kumeelezwa dhahiri.  “Na katika Torati karibu vitu vyote husafi rishwa kwa damu, na pasipo damu hakuna ondoleo.  Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafi shwe  kwa hizo(damu za wanyama);  lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafi shwe  kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.  Waebrania 9:22-23, yaani damu ya thamani ya Kristo.

Kutakaswa kwa Patakatifu Utakaso kwa kweli lazima utimizwe kwa damu ya Kristo.  

Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo”  Ondoleo au kuweka dhambi mbali ndiyo kazi inayotakiwa kukamilishwa.

 Lakini dhambi na mbingu huhusianaje?  

Jambo hili litaeleweka kwa kuchunguza huduma iliyokuwa ikifanyika katika patakatifu pa duniani, jinsi makuhani walivyokuwa wakihudumu. Waebrania 8:5.

Huduma ya patakatifu pa duniani ilikuwa na sehemu mbili.

  Makuhani walihudumu kila siku katika patakatifu wakati ambapo kuhani mkuu alihudumu mara moja kwa mwaka katika patakatifu mno.  

Huduma hiyo ya mara moja kwa mwaka iliitwa huduma ya upatanisho, ambayo ilihusu utakaso wa patakatifu.  Siku kwa siku mwenye dhambi aliyetubu alileta sadaka yake, akaweka mikono yake juu yake, akaungama makosa yake, ambayo ni sawa anahamisha dhambi zake na kuziweka kwa sadaka hiyo isiyo na hatia.  
Kisha mnyama huyo wa sadaka alichinjwa.  “Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu”  Lawi. 17:11.

 Sheria ya Mungu iliyovunjwa ilidai uhai wa mvunjaji.  Damu huwa badala ya uhai wa mwenye dhambi ambaye hatia yake imechukuliwa na yule mnyama wa sadaka.  
Basi kuhani alichukua damu hiyo mpaka patakatifu akainyunyiza  mbele ya pazia, ambalo hukinga sheria ya Mungu iliyovunjwa.  

Kwa huduma hiyo dhambi ilihamishwa na kuwekwa katika patakatifu.  Wakati mwingine damu haikupelekwa katika patakatifu, ila kuhani aliila nyama ya sadaka.  Mambo yote mawili, yaani kunyunyiza damu na kula nyama, yalifananisha jambo moja tu, ndiyo kuihamisha hatia kutokaa Kafara ya kondoo iliwakilisha kifo cha Kristo pale msalabani. kwa mwenye hatia na kuiweka katika patakatifu.  Kazi hiyo iliendelea daima mwaka mzima.  Dhambi za Waisraeli zilihamishwa namna hiyo na kuwekwa katika patakatifu, na hiyo ilikuwa kazi ya lazima ya kuhamisha dhambi zao.hapo tumeendelea kuona kama utangulizi wa somo hili ninakukaribisha tunapoendelea na sehemu inayofuata juu ya somo hili Karibu sana na Mungu akubariki sana.
Previous
Next Post »